Ghasia Afrika kusini: Watanzania 21 kurejeshwa, 3 wafariki dunia
Akizungumzia uamuzi huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe amesema watanzania 21 watarejeshwa nchini kutokana na vurugu zinazoendelea za wenyeji kuwashambulia wageni huko Afrika Kusini.
Ameongeza kuwa watanzania watatu wamefariki kwa maradhi lakini si kuuawa katika vurugu hizo, na kusisitiza kuwa hakuna mtanzania aliyeuawa kutokana na machafuko hayo.
Amesema habari zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuna watanzania waliokufa ni kweli il watanzania hao wamekufa katika matukio tofauti na vurugu hizo. Watanzania hao ni Athman China aliyefariki kwa kupigwa kisu gerezani, Rashidi mohamed aliyeuawa kilomita 90 toka tukio la uporaji pamoja na Ali Heshi Mohamed aliyekufa kwa ugonjwa wa TB kutokana na maelezo ya polisi nchini humo.
Katika hatua nyingine Waziri Membe amewataka watanzania kujiandikisha katika ubalozi Tanzania nchini humo ili serikali iweze kuwarejesha nchini wakati serikali ya Afrika kusini ikilishughulikia suala hilo.