Friday, 10 April 2015

Sakata la Gwajima: Polisi Wamhoji Kwa Masaa Matano..... Atakiwa Kurudi Polisi Wiki Ijayo na Hati ya Usajili wa Kanisa Lake,Helkopta na Viwanja Anavyomiliki

Sakata la Gwajima: Polisi Wamhoji Kwa Masaa Matano..... Atakiwa Kurudi Polisi Wiki Ijayo na Hati ya Usajili wa Kanisa Lake,Helkopta na Viwanja Anavyomiliki


Askofu wa  Kanisa la Ufufua na Uzima Josephat Gwajima amelitikisa  tena  Jiji la Dar es Salaam jana  mara   baada  kuwasili makao  makuu  ya  Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ili  kuendela  na  mahojiano kuhusu tuhuma za kumkashfu  Askofu Pengo.
 
Gwajima aliwasili  Makao Makuu ya Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Majira ya saa mbili kamili asubuhi huku akisindikizwa na viongozi mbali mbali wa Kanisa la Ufufuo na Uzama pamoja na Mwanasheria wake .
 
Eneo  lote  la  kituo  hicho  cha  polisi  lilikuwa  chini  ya  ulinzi  mkali wa maofisa mbalimbali wa Usalama wa Taifa wakisaidiwa na Jeshi la Polisi.
 
Baada  ya  kuwasili  kituoni  hapo, umati mkubwa  wa Waumini wake ulizunguka  maeneo yote ya  Kituo hicho   huku  wengine  wakiwa maeneo ya stendi ya Treni ya Reli ya kati.
 
Kama  kawaida, Waumini  hao walikuwa  wakiimba nyimbo mbalimbali ambazo wanadai zilikuwa  mahususi  kumpa nguvu Askofu huyo ajibu kesi hiyo kwa ufasaha.
 
Baada  ya  Mahojiano  ya  takribani  masaa  Matano, hatimaye   Askofu Gwajima  alitoka  ndani  ya kituo  hicho,lakini  katika  hali  isiyo  ya  kawaida,Askofu  huyo  aligoma kuongea na vyombo vya habari.
 
Baada  ya  Gwajima  kugoma  kuongea,mwandishi wetu  alimfuata Mwanasheria  wake  aliyekuwa  ameambatana  naye,John Mallya  ambaye alisema kuwa  mteja  wake  alikuwa  amechoka, hivyo  asingeweza  kuongea.

Mallya  alimweleza  mwandishi kuwa  mambo aliyohojiwa  Gwajima   ni kuhusu mali zake na sio matamshi ya kumtukana Askofu  Pengo.
 
“Mahojiano yamekwenda vizuri lakini nasikitika sana kutokana na mambo waliyokuwa wanamhoji. Wamemuuliza mambo ambayo hayahusiani kabisa na kile tulichotarajia na ndicho kilichotuleta hapa, nilidhani mteja wangu ataulizwa kuhusiana na matumizi ya lugha chafu iliyodaiwa kutumika kumkashifu kiongozi mwenzake wa dini,” alihoji wakili wa Gwajima.
 
Aliendelea kusema kuwa, mambo aliyoulizwa ni kuhusiana na ukoo wake, wazazi wake hata ndugu zake na watu wengine wa kwao waliokufa.
 
Alisema walihoji pia juu ya mambo mengine kama umiliki wa helikopta, utajiri wake, nyumba anayoishi, uhusiano wake na watu mbalimbali.
 
“Nimeshangaa sana kuona mteja wangu ameulizwa vitu kama hivyo ambavyo havihusiani na madai ya hapo awali ya matumizi ya lugha ya matusi. Tumeagizwa tulete nyaraka kumi siku ya mahojiano yetu tena yatakayofanyika tarehe 16 mwezi huu na sisi tutafanya hivyo,” alisema Mallya.
 
Alizitaja nyaraka na vitu vingine wanavyotakiwa kuvipeleka Aprili 16 ni hati ya usajili wa kanisa, bodi ya udhamini wa kanisa na majina yao, idadi ya makanisa yaliyopo chini yake, na muundo wa uongozi wa kanisa lake.
 
Vingine ni namba ya usajili wa kanisa, ritani za kanisa lake (mapato na matumizi ya fedha za kanisa lake), mtu anayechukua na kurekodi mkanda wa video kanisani kwake, pamoja na waraka wa Baraza la Maaskofu uliosomwa makanisani.

clouds stream