Wanajeshi kudhibiti ghasia dhidi ya wageni Afrika Kusini
Wanajeshi wanafanya doria katika baadhi ya majimbo ya Kwa-Zulu Natal na Gauteng, pia mjini Alexandra uliopo jiji la Johannesburg ambako Raia wa Msumbiji aliuawa na wengine raia wengine kadhaa kutoka Zimbabwe walinusurika na shambulio.
Watu wameonekana katika makundi wakiwa wamebeba mishumaa karibu na jengo la Mahakama kuu mjinin Johannesburg wakitoa wito wa kukomesha machafuko,ambayo yamegharimu maisha ya watu saba.
Historia ya nchi hiyo inaonyesha kuwa nnamo mwaka 2008, Jeshi la Afrika kusini lilisambazwa nchini humo baada ya Watu 63 kuuawa kutokana na mashambulizi ya wenyeji dhidi ya wageni.