Rais wa Nigeria anusurika kwenye mlipuko wa bomu
Mtu mmoja amefariki na wengine
18 wamejeruhiwa vibaya sana baada ya mwanamke aliyekuwa na bomu
kujilipua kwenye sehemu ya kuegeshea magari muda mchache baada ya hotuba
ya Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan, aliyekuwa ameondoka eneo la tukio
muda mchache. Licha ya kikundi cha Boko Haram kutoongea chochote kuhusu
mlipuko huo, kwenye tukio hilo ambalo mwanamke huyo alikufa haphapo
baada ya mlipuko.
Nigeria ipo mbioni kuelekea uchaguzi
mkuu huku, na Rais Goodluck yupo katika harakati za kampeni za
kuchaguliwa kuiongoza nchi hiyo tena licha ya kushutumiwa kushindwa
kulimaliza suala la Boko haramu. Mlipuko wa leo ulitokea mjini Gombe
alikokuwa anapiga kampeni zake.