Wednesday, 13 May 2015

Bungeni: Pinda ataja sababu za mauaji ya Albino

Bungeni: Pinda ataja sababu za mauaji ya Albino



Waziri  Mkuu  wa Tanzania Mh.  Mizengo Pinda.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda.
Waziri  Mkuu  wa Tanzania Mh.  Mizengo Pinda amezitaja sababu zinazopelekea kukithiti kwa mauaji ya Albino nchini Tanzania yaliyopelekea  watu wenye aualbino kuuawa pamoja na kupoteza viungo mbalimbali vya mwili.
Akizungumza katika  kikao cha bunge la Bajeti 2015/2016 leo mjini Dodoma Mh. Pinda amesema mwaka 2010 kulikuwa na tukio moja la mauaji ya albino, 2011 hapakuwa na tukio la mauaji, 2012 tukio moja, 2013 tukio moja, 2014 matukio manne na mwaka 2015 tukio moja.
Takwimu hizo zinaonesha kwamba 2006-2015 jumla  ya wenye ulemavu wa ngozi  43 wameuawa kutokana na vitendo hivyo vya ukatili. Suala hilo limesababisha watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na familia zao kuishi kwa hofu na  mashaka kushindwa kushiriki  kikamilifu  katika shughuli  za maendeleo.
Vitendo hivyo, vimeleta  taswira isiyo nzuri kwa nchi ya Tanzania kwa kuwa watu wengi nje ya nchi wana amini watanzania wananishi kwa upendo na  amani.
Katika kupambana na  kuatili huo,jumla ya watuhumiwa 181 walikamatwa na kuhojiwa kati ya mwaka 2006 hadi 2015, kati yao wautuhumiwa 133 wamefikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi za mauaji na 46 kwa makosa ya kujeruhi.
Wathumiwa 13 wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa na mtuhumiwa 1 amehukumiwa kifungo cha miaka 20 kwa kosa la kujeruhi na watuhumiwa 73 wameachiwa huru na mahakama kwa kukosa ushahidi. Wathumiwa  6 hawajakamatwa  na  upelelezi  wa kesi kumi bado unaendelea. Watuhumiwa wawili waliuawa na wananchi wenye hasira kali.
Akizungumzia  chanzo  cha mauaji hayo  Mh. Pinda amesema  chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina, huku  baadhi ya watu wakiamini viungo hivyo vitawapa mafanikio au vyeo, mali au utajiri.
Amesisitiza kuwa utajiri hauwezi kupatikana kwa njia haramu kama hizo, utajiri unapatikana kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na sio vinginevyo huku akiyataka   mashirika ya dini kuwaelimisha wananchi dhidi kuondoa imani potofu.

clouds stream