Monday, 18 May 2015

Nkurunziza atoa onyo kwa Al shabaab, Wamarekani watimka Burundi

Nkurunziza atoa onyo kwa Al shabaab, Wamarekani watimka Burundi

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi.
Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi.
Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi amejitokeza kwa mara ya kwanza tangu jaribio la mapinduzi la jumatano iliyopita.
Rais Nkurunziza akihutubia waandishi wa habari katika ikulu ya Bujumbura alionya kuwa kuna tishio la shambulizi la kigaidi kutoka kwa kundi la waislamu kutoka Somalia wenye uhusiano na Al-Qaeda , Al Shabaab.
Aliwaambia wandishi wa habari wa kimataifa kuwa tishio hilo la mashambulizi sio tu kwa taifa lake bali pia kwa Kenya na Uganda .
Hata hivyo, Nkurunziza hakuzungumzia lolote kuhusu hali ilivyo nchini Burundi wala tishio la mapinduzi dhidi yake.
Kwa upande wa Wapinzani wake  wanasema huenda hiyo ni njama ya rais Nkurunziza kuidhinisha makabiliano makali dhidi ya wapinzani wake ambao tayari wameagiza wafuasi wao kujitokeza kwa wingi hapo kesho kuendelea na maandamano ya kumtaka asiwanie kipindi cha tatu katika kura za urais zitakazofanyika mwezi
Tishio la Al Shaabab dhidi ya Burundi li kufuatia mchango wake katika jeshi la umoja wa Afrika Amisom huko Somalia.
Marekani tayari imeagiza raia wake kuondoka nchini humo kufuatia tishio la shambulizi la kigaidi mbali na kuzorota kwa hali ya usalama.

clouds stream