Majanga yaikumba Nepal, watu wengine 40 wafa kwa tetemeko
Mvua kubwa iliyoambatana na tetemeko kubwa nchini Nepal imesababisha watu 40 kufariki dunia. Wakuu nchini humo wamethibitisha kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana na tetemeko hilo jipya , imepanda na kufikia zaidi ya watu 40.
Wakati huo huo helkopta ya kikosi cha majini ya Marekani,ambayo ilikuwa ikifanya kazi ya kusaidia kusambaza huduma za kibinaadamu nchini Nepal, haijulikani.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa, ndani ya helkopta hiyo kulikuwa na watu nane,miongoni mwao, sita ni askari wa kikosi cha majini cha Marekani na askari wawili wenyeji wa jeshi la Nepal.
Maofisa wa serikali wa Marekani wamesema kwamba helkopta hiyo ilikuwa maeneo ya jirani na kijiji cha Charikot, ambacho kiliharibiwa vibaya na tetemeko la ardhi.