Rais Nkurunzinza ”apinduliwa” Burundi
Meja Generali Niyombareh aliyetimuliwa nchini Burundi ametangaza rasmi kuwa hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa Burundi.
Amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.
Wakati akitangaza uamuzi huo Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la nchini Burundi.
Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi itakayotawala taifa hilo kwa kipindi cha mpito.
Habari kutoka Burundi zimebainisha kuwa raia wengi wamejitokeza barabarani huku wakishangilia kauli hiyo ya ”Mapinduzi”.
Kwa sasa rais Nkurunziza yuko nchini Tanzania alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda ya Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.