Thursday, 28 January 2016

Magufuli Amteua Banzi Naibu Gavana Benki Kuu

Magufuli Amteua Banzi Naibu Gavana Benki Kuu

Tarehe January 28, 2016
Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, amemteua Ndugu Julian Banzi Raphael, kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imebainisha kuwa kabla ya uteuzi huu Ndugu Julian Banzi Raphael alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara na Viwanda, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Ndugu Julian Banzi Raphael anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Juma Reli ambaye muda wake umemalizika tarehe 12 Julai, 2015.

CUF Wagoma, CCM ‘Mbele Kwa Mbele’ Uchaguzi Mkuu Zanzibar

CUF Wagoma, CCM ‘Mbele Kwa Mbele’ Uchaguzi Mkuu Zanzibar

Tarehe January 28, 2016
Rais wa Zanzibar.Dk.Shein pamoja na Makamu wa Rais Zanzibar Maalim Seif (kulia).
Rais wa Zanzibar.Dk.Shein (Kushoto) pamoja na Makamu wa Rais Zanzibar Maalim Seif (kulia) ambao ni wagombea wenye upinzani mkubwa Visiwani Zanzibar.
Chama cha Wananchi (CUF) kimetangaza rasmi kutoshiriki marudio ya uchaguzi wa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika Machi 20 mwaka huu huku Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiwataka wanachama wake kujiandaa kwa uchaguzi wa marudio.
Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Hamad amewaambia waandishi wa habari leo kuwa baada ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF kujadili tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha, la kuitisha uchaguzi wa marudio tarehe 20 Machi, wametoa azimio la kukataa moja kwa moja kushiriki uchaguzi huo waliouita ‘batili’.
“Chama Cha Wananchi (CUF) hakitoshiriki katika uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2016 kwa sababu uchaguzi huo si halali kwani uchaguzi halali ulishafanyika,” imesomeka sehemu ya maazimio hayo.
Baraza hilo limesema uchaguzi mkuu wa Zanzibar ulikwishafanyika tarehe 25 Oktoba 2015 na washindi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani  kupewa shahada za kuwathibitisha na kuwatambua kama washindi halali.
CUF wameziomba jumuiya za kimataifa na taasisi zinazosimamia haki za binadamu na zinazopambana na makosa ya jinai kimataifa ikiwemo Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (International Criminal Court – ICC) kufanya uchunguzi wa hali ilivyokuwa wakati wa uchaguzi ili kupata majibu ya kinachoendelea visiwani Zanzibar.
Vilevile baraza hilo limetoa wito kwa wazanzibari kutoshiriki uchaguzi huo usio halali wa marudio.

Baada Ya Kuitandika Everton,Man City Waingia Fainali Na Liverpool


Baada Ya Kuitandika Everton,Man City Waingia Fainali Na Liverpool


Tarehe January 28, 2016
Mshambuliaji wa Manchester City Kun Aguero akishangilia baada ya kuifungia goli timu yake
Mshambuliaji wa Manchester City Kun Aguero akishangilia baada ya kuifungia goli timu yake

Man City imekua timu ya pili kufuzu fainali ya mchezo wa kombe la Capital baada ya kuichapa Everton kwa mabao 3-1.
Everton ndio walikua wa kwanza kuzifumani nyavu za Man city baada ya kiungo Ross Barkley kuifungia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 18 ya mchezo.
Kiungo wa kibrazl Fernandinho akasawazisha bao hilo kwa shuti kali baada ya kutoka piga nikupige kwenye goli la everton katika dakika ya 25.
Kevin De Bruyne akaongeza bao la pili baada ya kunganisha krosi ya kutoaka upande wa kushoto iliyopiga na Raheem Sterling, kina Sergio Aguero kun, akahitimisha kazi kwa bao la tatu.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Goodson Park Everton walishindwa kwa ushindi wa mabao 2-1,Man City watachuana na Liverpool katika mchezo wa fainali utaofanyika februari 28 katika dimba la la Wembley.

Monday, 18 January 2016

Wakazi Mkwajuni Wafunga Barabara Kupinga Bomoa Bomoa

Wakazi Mkwajuni Wafunga Barabara Kupinga Bomoa Bomoa

Tarehe January 18, 2016
Jeshi la Polisi likitoa msaada katika barabara iliyotokea vurugu katika Bonde la Mkwajuni leo.
Jeshi la Polisi likitoa msaada katika barabara iliyotokea vurugu katika Bonde la Mkwajuni leo.
Wananchi  ambao makazi yao yamebomolewa  katika Bonde la Mto mkwajuni leo wamefunga barabara ya Kinondoni Kawe katika Bonde la Mkwajuni  na kusababisha usafiri wa daladala na magari mengine kusimama kwa muda.
Kwa mujibu wa wakazi wa Bonde hilo wameiambia Hivisasa kuwa wamechukua hatua  ya kufunga barabara hiyo kufuatia kukerwa na zoezi la Bomoa bomoa lililotekelezwa na serikali na kuwaacha wakiwa hawana mahali pa kwenda.
Licha ya wananchi hao kuzuia barabara hiyo, Jeshi la Polisi Manispaa ya Kinondoni limefika katika eneo  hilo na  kuwazuia wananchi waliokuwa wamechoma matairi ya gari katikati ya barabara.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi  waliamua kukimbia mara baada ya kuona magari ya Jeshi la Polisi katika eneo hilo.

Barabra iliyofungwa na wananchi.
Barabara iliyofungwa na wananchi.
Baadhi ya wananchi wakiangalia kinacho endelea mara baada ya barabara ya kufungwa.
Baadhi ya wananchi wakiangalia kinacho endelea mara baada ya barabara  kufungwa kutokana na Vurugu.

Mhariri Mkuu Afunguka Kufutwa Gazeti La Mawio


Mhariri Mkuu Afunguka Kufutwa Gazeti La Mawio


Tarehe January 18, 2016
.
1 (2)

Mhariri Mkuu wa gazeti la Mawio  ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Victoria Media inayolimiliki gazeti hilo Bw. Simon Mkina ameeleza jinsi walivyopokea taarifa ya kufungiwa gazeti lake Maisha.
Adha, Jana Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye alitangaza  kuwa gazeti hilo limefutwa kutokana na kuandika habari za uchochezi na zenye utata na kwamba wamiliki wa gazeti hilo wamekuwa wakionywa na serikali tangu mwaka 2013 lakini hata majibu yao yalikuwa ya kiburi na dharau.
Akizungumzia hatua hiyo  Mkina amesema kuwa ingawa wamekuwa wakisikia habari za kufutwa kwa gazeti lao kweye vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii, bado hawajapata taarifa rasmi kutoka serikalini kuhusu uamuzi huo ili wajue hatua watakazoweza kuchukua.
Amesema kuwa uongozi wa kampuni hiyo umepanga kukaa na kufikiria hatua sahihi za kuchukua kutokana na uamuzi huo na kuitaka serikali kuwapa taarifa ya maandishi kuhusu sababu zilizopelekea kufutwa kwa gazeti lao na habari iliyosababisha wafutwe.
Ameongeza kuwa Kampuni yake  inashindwa kufahamu ni habari gani ilisababisha wafutwe kwa kuwa walikuwa wakipokea barua ya kujieleza karibia kila baada ya wiki mbili kuhusu habari walizokuwa wanaziandika.

Sahara Media Group Yaijibu TCRA, Kufungiwa Star Tv

Sahara Media Group Yaijibu TCRA, Kufungiwa Star Tv

Tarehe January 17, 2016
Anthony Diallo mmiliki wa Kampuni ya Sahara Media Group.
Anthony Diallo mmiliki wa Kampuni ya Sahara Media Group.
Kampuni ya Sahara Media Group inayomiliki   Star Tv, RFA  na Kiss Fm  imebuka na kuishangaa  mamlaka ya mawasilano Tanzania TCRA  iliyoitaka  kampuni hiyo kufunga vyombo vyake vyote vya habari.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na TCRA imevitaja vyombo vya habari 21 ikiwemo Star TV, Redio Free Afrika na Kiss FM kwa madai ya kutolipia ada ya leseni.
Wakizungumzia  kufungiwa na TCRA Manejimenti ya sahara media group  imesema kuwa haijapata barua au taarifa rasmi yeyote kutoka TCRA  ya kutakiwa kufunga vyombo vyake.
Imesema wameshtushwa na taarifa hiyo ikizingatiwa kwamba wamekuwa wakilipia leseni ada zake na ada za masafa kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 500 hadi kufikia mwezi October 2015.
Wamesema yamekuwapo mawasiliano ya mara kwa mara kati ya TCRA kanda ya Mwanza, makao makuu na sahara media group limited nakukubaliana juu ya utaratibu wa malipo ya ada husika.
Hata hivyo  menejimenti imeshangazwa na hatua hiyo ya TCRA kutangaza kuvifungia vituo vyake kupitia mkutano wa  vyombo vya habari bila kujali athari za kufungia vyombo vya kitaifa kwa walaji na watoa huduma.
Sahara media group limited imekuwa ikilalamikia utozwaji wa ada kwa dola za kimarekani jambo ambalo limekuwa likipandisha ada hizo kila mara na kufanya ulipwaji wa ada hizo kibajeti kukwama kwama.
Menejimenti pia imelaani taarifa hiyo kutolewa mwishoni wa wiki na kuvipa vituo husika siku mbili tu kukamilisha ulipaji ada wakijua dhahiri jumamosi na jumapili sio siku za kazi.
Menejimenti ya star tv  imewaondoa wasiwasi watazamaji na wasikilizaji wake  kufuatia  kuanza kulishughulikia suala hilo kati yake na TCRA.

Thursday, 14 January 2016

Kipindupindu Chaitesa Simiyu, Wanne Wafa, 85 Waugua

Kipindupindu Chaitesa Simiyu, Wanne Wafa, 85 Waugua

Tarehe January 14, 2016
kipindupindu
Watu wanne wamekufa wilayani Bariadi mkoani Simiyu kutokana na ugonjwa wa kipindupindu na wengine 85 wameugua na kutibiwa, huku kambi saba zikitengwa kwaajili ya wagonjwa katika wilaya za Busega na Bariadi.
Akizungumzia mlipuko wa ugonjwa huo daktari mwandamizi kitengo cha dharura na maafa wizara ya afya, maendeleo ya jamiii, jinsia, wazee na watoto, Dr Mary Kitambi amesema kufuatia kuongezeka kwa wagonjwa wa kipindupindu imewalazimu kufika mkoani Simiyu ili kuhakikisha wanashirikiana na mkoa katika kutokomeza ugonjwa huo kwa kuihamasisha jamii kuzingatia usafi.
Mwakilishi wa shirika la afya duniani WHO nchini Zambia, Nora Mwemba ambaye ameambatana na watalaam toka wizara ya afya amesema amekuja nchini ili kuongeza nguvu ya utoaji wa elimu pamoja na mahitaji ya dawa kwa wahudumu wa afya ili jamii iweze kuelewa na kuondokana na ugonjwa huo.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Simiyu, Eraston Mbwilo aliyetembelea wagonjwa katika kambi ya Dutwa wilayani Bariadi na Chamugasa wilayani Busega ameagiza kila  kaya inazingatia usafi kwa kunawa kabla na baada ya kula, huku akiwaagiza wakuu wa wilaya ya Busega na Bariadi kukutana kwaajili ya kuweka mpango mkakati wa kudhibiti mlipuko huo.

Real Madrid Na Atletico Madrid Wapigwa Marufuku Kununua Wachezaji

Real Madrid Na Atletico Madrid Wapigwa Marufuku Kununua Wachezaji

Tarehe January 14, 2016
Christiano Ronaldo wa Real Madrid
Christiano Ronaldo wa Real Madrid
Miamba wa Uhispania Real Madrid na Atletico Madrid wamepigwa marufuku kutonunua wachezaji wapya sokoni vipindi viwili.
Klabu hizo zimeadhibiwa na shirikisho la soka duniani Fifa kwa kukiuka sheria za uhamisho wa wachezaji kuhusu kununuliwa kwa wachezaji ambao bado ni watoto.
Marufuku hiyo haitaathiri kipindi cha sasa cha kununua wachezaji, ambacho kinaendelea hadi mwisho wa mwaka huu.
Atletico pia wametozwa faini franka 900,000 za Uswizi ambazo ni sawa na pauni 622,000 za Uingereza, nao Real wakatakiwa kulipa franka 360,000 (£249,000).

URA Mabingwa Wapya Mapinduzi Cup

URA Mabingwa Wapya Mapinduzi Cup

Tarehe January 14, 2016
Kikosi cha mabingwa wa michuano ya mapinduzi Timu ya URA kutoka Uganda
Kikosi cha mabingwa wa michuano ya mapinduzi Timu ya URA kutoka Uganda
Timu ya URA kutoka Uganda imeibuka na ubingwa wa kombe la mapinduzi katika fainali iliyomalizika mapema jana kwa kuitandika Mtibwa Sugar jumla ya mabao 3-1.
Mtibwa wanaandika histori nyingine ya kulikosa kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo ambapo mwaka jana waliingia fainali na Simba na kulipoteza kombe hilo .
Bao la kwanza lililofungwa na Julius Ntambi kwa kichwa, lilidumu hadi mwisho wa dakika 45 na timu ziliporejea uwanjani ilionekana kama Mtibwa Sugar wamejiandaa kusawazisha
Hata hivyo, mambo hayakuwa mazuri baada ya kufungwa mabao mengine harakaharaka yakifungwa na David Lwasa aliyeingia kipindi cha pili ambaye alitumia makosa mara mbili ya mabeki wa Mtibwa Sugar ambao mwishoni walionekana kuchoka.
Bao pekee la Mtibwa Sugar lilifungwa dakika ya 90 na Jaffar Salum baada ya kipa wa URA kufanya mzaha na mfungaji akampokonya mpira na kuutupia wavuni.

Nape Alia Na Lowassa, Ataka Chadema Imngo’e

Nape Alia Na Lowassa, Ataka Chadema Imngo’e

Tarehe January 14, 2016
Mwanasiasa Edward Lowassa.
Mwanasiasa Edward Lowassa.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amekitaka chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimfukuze aliyekuwa mgombea urais Edward Lowassa ili kuonesha kuwa kweli wana dhamira ya dhati ya kupambana na ufisadi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini hapa Nape alisema  Chadema waliachana na ajenda ya ufisadi mara baada ya kumpokea mwanasiasa Edward Lowassa aliyekuwa anatuhumiwa kwa ufisadi katika sakata la Richmond.
Amesema CCM haikumpitisha Lowassa kugombea urais kwa sababu ya ufisadi sababu iliyopelekea aamue kuhama CCM na kutimkia Chadema.
Nape amesema hayo akimjibu Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu ambaye juzi alisema kuwa ufisadi ni ajenda ya kudumu ya Chadema kwa madai kuwa Rais Magufuli hawezi kuufumua wote katika uongozi wake.
Katibu huyo wa Itikadi amesema ajenda ya ufisadi ndiyo ilikibeba chama hicho katika uchaguzi mkuu ndio sababu ya Dkt. John Magufuli kuibuka mshindi akimuacha kwa mbali mpinzani wake Edward Lowassa.

CCM Waibua Mbinu Mpya Kuimaliza Ukawa 2016

CCM Waibua Mbinu Mpya Kuimaliza Ukawa 2016

Tarehe January 13, 2016
Mwenyekiti wa CCM Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa CCM Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kipo katika mpango kabambe wa kujiimarisha mara ya kupata misuko suko katika uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba  25,2015 ambapo Wanachama wake walijiondoa na hivyo kuleta mpasuko ndani ya chama hicho.
Miongoni mwa wanasiasa walio jitoa katika chama hicho  hali iliyopelekea kuondoka na wanachama wa CCM ni aiyekuwa Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu mstaafu  Edward Lowassa,Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye na kada mkongwe ndani ya chama hicho Mzee Kingunge Ngombale Mwiru.
Makada hao walileta mtikisiko ndani ya chama cha Mapinduzi huku watafiti wa masuala ya kisiasa wakishidwa kubashiri nani angeibuka mshindi katika kiti cha Urais  ambapo licha ya mchuano mkali  Mgombea wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli aliibuka kidedea na kumshinda Edward  Lowassa kwa asilimia 58.46 huku lowassa akiambulia  asilimia  39.97.
Baada ya kutangazwa mshindi  wa Urais Dkt. John Pombe Magufuli alianza kazi kwa kasi kubwa na kuahid kutumbua majipu yaliyokwamisha mipango mbalimbali ya serikali kutokana na upotevu wa mapato katika sekta za umma ikwemo Bandarini na Mamlaka ya Mapato pamoja na kuwaondoa watendaji wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma na kuundoa mfumo wa kufanya kazi kwa mazoea.
Ikiwa ni miezi 2 imepita tangu Magufuli aanze kazi, kasi yake imeonesha kuwamaliza nguvu wapinzani ambao mara kwa mara wamekuwa wakidai kwamba kiongozi huyo wa CCM anatekeleza sera zao huku baadhi ya wananchi wakihoji sera za upinzani kwa sasa baada ya ile ya ufisadi kuwa haina mashiko tena mbele ya jamii.
Mwaka huu wa 2016 ifikapo  februari 05 Chama hicho  kitakuwa kinatimiza miaka 39 tangu kuzaliwa kwake mwaka 1977.
Hivyo Chama hicho kinatarajia kufanya maadhimisho ya aina yake pamoja na kuja na mipango kabambe  ya kujiimarisha ili kuvipunguza  nguvu vyama vya Upinzani  ikiwemo Chadema na CUF.
Kwa mujibu wa taarifa yake Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na uenezi Nape Moses Nnauye (Mb) amesema kwamba sherehe hizo kwa mwaka huu zitakuwa za aina yake kufuatia kuweka malengo katika Ujenzi wa Chama kwa kuzoa wanachama wapya katika maeneo mbalimbali nchini.
Ujenzi huo wa chama utahusisha, Kuingiza wanachama wapya wa CCM na Jumuiya zake na kufanya shughuli nyingine za kuimarisha Chama, kufanya mikutano ya kuwashukuru wana CCM na wananchi kwa kuiamini CCM kuendelea kuongoza Nchi, kushiriki na kukamilisha Uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo CCM ilipata ushindi wa kishindo wa Rais, Wabunge na Madiwani pamoja na  kuhamasisha wananchi kufanya kazi ili kujiletea maendeleo yao binafsi na ya Taifa.
Shughuli nyingine ni  kushiriki shughuli za maendeleo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa, zahanati, vituo vya afya, upandaji miti, uchimbaji wa mitaro ya maji, kufanya usafi wa mazingira pamoja na shughuli nyingine za kijamii.
Kaulimbiu ya sherehe hizo ni Sasa Kazi, Kujenga Nchi na Kukijenga Chama”.
Aidha,Uzinduzi wa maadhimisho ya kumbukumbu ya hiyo utafanyika tarehe 31 Januari, 2016 Unguja, Zanzibar ambapo Mgeni rasmi atakuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar, Dokta Ali Mohammed Shein.
Kwa upande wa  Kilele cha maadhimisho hayo  kitakuwa ni  Februari 06, 2016 mjini Singida ambapo Mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete.

Sunday, 10 January 2016

Madereva Mwendokasi Waagoma Kisa Mshahara

Madereva Mwendokasi Waagoma Kisa Mshahara

Tarehe January 11, 2016
Mradi wa mabasi yaendayo kasi.
Mradi wa mabasi yaendayo kasi.
Mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi uliopangwa kuanza kazi leo na kusitishwa kutokana na kutokamilika kwa pendekezo la nauli,madereva wake wamegoma kufuatia uongozi wa mabasi hayo kuwapa mkataba wa kazi usiokidhi mahitaji.
Kwa mujibu wa madereva hao wamesema kwamba wamegoma kutokana na kupewa mkataba wenye mshahara mdogo ambao ni shilingi shilingi laki 4  huku makubaliano ya awali ya shilingi laki 8.
Madereva hao wamesema pia wameshangazwa na kitendo cha uongozi wa mabasi hayo kuwapa mkataba wa kazi bila ya kuwapatia nakala yake jambo ambalo wamesema ni kinyume cha taratibu za ajira.
Mgomo huo umetokea kituo kikuu cha mabasi yaendayo haraka kilichopo eneo la Kamata jijini Dar es salaam.

Matokeo Mechi Zote FA Cup Angalia Hapa

Matokeo Mechi Zote FA Cup Angalia Hapa

Tarehe January 11, 2016
Kocha wa Arsenal,Arsen Wenger
 
CardiffShrewsbury 0 : 1
TottenhamLeicester2 : 2
CarlisleYeovil2 : 2
Chelsea Scunthorpe2 : 0
Oxford Utd Swansea3 : 2
Manchester United Sheffield Utd1 : 0
Arsenal Sunderland3 : 1
BirminghamBournemouth 1 : 2
BrentfordWalsall 0 : 1
BuryBradford0 : 0
Colchester Charlton2 : 1
DoncasterStoke City 1 : 2
EastleighBolton1 : 1
Everton Dagenham & Red.2 : 0
HartlepoolDerby 1 : 2
HuddersfieldReading2 : 2
Hull City Brighton1 : 0
IpswichPortsmouth2 : 2
Leeds Rotherham2 : 0
MiddlesbroughBurnley 1 : 2
NorthamptonMilton Keynes Dons2 : 2
NorwichManchester City 0 : 3
Nottingham QPR1 : 0
Peterborough Preston2 : 0
Sheffield Wed Fulham2 : 1
SouthamptonCrystal Palace 1 : 2
Watford Newcastle Utd1 : 0
West BromBristol City2 : 2
West Ham Wolves1 : 0
WycombeAston Villa1 : 1

clouds stream