Monday, 25 September 2017

Msigwa ‘Akabana Koo’ Na Polisi

Related image
Mchungaji Msigwa Mbunge wa Iringa mjini.

Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amesema atalishitaki Jeshi la Polisi, kwa tuhuma za kuingilia
majukumu yake ya kikazi pale anapokuwa akitimiza wajibu wake wa kibunge ikiwemo kuongea na wananchi.
Mchungaji Msigwa amesema hayo kufuatia zuio kutoka Jeshi la Polisi linalomtaka kutoendelea na mikutano yake ya hadhara katika
kata za Mkoani humo hado pale Jeshi hilo litakaposema vinginevyo saa chache baada ya kumkamata akiwa jukwaani kwa tuhuma
za uchochezi kwa madai ya kukiuka masharti alipohutubia katika Kata ya Mlandege.
Amesema hatahivyo atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo kwani alitarajia kufanya mikutano katika kata za Kihesa na Kitwiru
Mchungaji Msigwa amesema chombo pekee kinachoweza kumtia hatiani kwa kufanya uchochezi ni Mahakama na sio polisi.
“Walinikamata tangu saa 11:30 na kuanza kunihoji mpaka saa 3:15 usiku kwa tuhuma za kufanya uchochezi lakini mimi nakataa
sijafanya uchochezi kwa sababau hakuna mtu anaweza kunizuia kuongea na wananchi wangu, wanadai nimeleta hofu na
kuvichonganisha vyombo vya dola na wananchi,” amesema Mchungaji Msigwa .
Amesema kwasasa yupo nje kwa dhamana na tayari ameripoti polisi asubuhi jana Jumatatu, amehojiwa lakini ameambiwa ataitwatena kwa mahojiano zaidi.
“Mimi niko tayari hata kama wangeniweka ndani wiki mbili siogopi kwa sababu sitanyamaza nitaendelea kuongea na sitaacha
kusema kilichomtokea Tundu Lissu na ili kuninyamazisha ni lazima waniue kwa sababu nishajiandaa kisaikolojia,” amesema
Mchungaji Msingwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi amesema walimkamata Msigwa kwa kuwa alikuwa anatoa maneno ya uchochezi
kwa wananchi aliokuwa anawahutubia mkutano wa hadhara Kata ya Mlandege.
Kamanda Mjengi amesema bado jeshi hilo linaendela na upelelezi juu ya tuhuma hizo na mara utakapokamilika watamfikisha
mahakamani Mbunge Msigwa.

clouds stream