Thursday, 7 September 2017

CHAMA CHA KENYATTA CHAPINGA KUFUMULIWA TUME YA UCHAGUZI

Uhuru Kenyatta.
Uhuru Kenyatta.
IMG-20170426-WA0006

Chama cha Jubilee, cha rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kimepinga kundi la Vigogo tisa wakuu wa Tume ya Uchaguzi nchini humo ambao wanatarajiwa kusimamia uchaguzi mpya mwezi ujao.

Chama hicho kimetoa orodha ya majina ya maafisa hao ambao kinasema wanajulikana kwamba “wanapendelea upande fulani”.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC alitangaza kundi la maafisa saba watakaoongoza maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika tarehe 17 Oktoba siku ya Jumanne.

Maafisa hao ambao wanajumuisha mkuu wa kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) na msimamizi wa kituo cha taifa cha kujumlishia matokeo watafanya kazi kwa miezi mitatu.

Chama cha Jubilee kimesema: “Tuna habari za kuaminika kwamba kwenye orodha ya maafisa hao (watakaosimamia uchaguzi) kuna watu wanaofahamika wazi kuegemea upande Fulani.”

Mahakama ya Juu imefuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti ambapo Rais Kenyatta alitangazwa mshindi kwa madai kuwa Tume ya Uchaguzi IEBC haikuandaa uchaguzi huo kwa njia na kwa kiwango kinachokubalika kikatiba.

clouds stream