Tuesday 26 September 2017

WAFUASI WA ODINGA WAINGIA BARABARANI




Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka Kenya ‘IEBC’, Ezra Chiloba amedaiwa kutangaza kuachia ngazi leo huku
wafuasi wa Muungano wa Upinzani (NASA) wakifanya maandamano katika baadhi ya maeneo nchini humo kushinikiza
kuondolewa kwa maafisa 12 wa tume hiyo akiwemo Ofisa Mtendaji Mkuu wa IEBC kwa shutuma za kuvuruga uchaguzi wa Agosti8, mwaka huu.
Maandamano hayo yaliyotawaliwa na ghasia katika baadhi ya maeneo ni mwitikio wa wito uliotolewa jana na Kiongozi wa
Upinzani, Raila Odinga aliyewataka wafuasi wake kujitokza kwa wingi kuandamana hadi Makao Makuu ya IEBC, ikiwa ni siku
chache tu zimepita tangu Mahakama ya Juu Kenya kufutilia mbali matokeo ya urais yaliyompa ushindi Rais Kenyatta.
Wafuasi wa NASA walikuwa wakimshutumu Chiloba na watendaji wengine kufanya njama za kuingilia mchakato wa uchaguzi huo
na kumsaidia Rais Kenyatta kuibuka kidedea.
Waandamanaji hao wamebeba matawi ya miti, mabango, huku wakipiga mayowe na honi za pikipiki kuanzia barabara ya Obote,
kasha mtaa wa Oginga Odinga kabla ya kuchukua barabara kuu ya Kenyatta hadi Mtaa wa Ang’awa katikati ya Jiji la Nairobi huku
watu wachache wakiwa wametiwa nguvuni na Jeshi la Polisi.
Haya yanajiri ikiwa ni siku 30 tu zimesalia hadi kufanyika uchaguzi wa marudio, Oktoba 26, mwaka huu.

clouds stream