Tuesday, 5 September 2017

Wabunge UKAWA Wasusia Kuapishwa Kwa Wabunge Wa CUF

Related image

Wabunge kutoka Upinzani katika Umoja wa Ukawa leo asubuhi wametoka nje ya Bunge na kususia shughuli ya kuapishwa kwa wabunge 7 wa Viti Maalum CUF.

Shughuli ya kuapishwa kwa wabunge hao imefanyika leo na Spika Job Ndugai kabla ya kuanza kwa kipindi cha maswali na majibu katika Mkutano wa 8 Bunge la 11.

Wabunge hao waliteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuziba nafasi ya wabunge nane wa Viti Maalum CUF waliotimuliwa uanachama na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.

Mmoja wa wateule hao, Bi. Hindu alifariki dunia siku chache kabla ya kuapishwa na hivyo kufanya idadi ya wabunge waliokula kiapo leo kuwa saba badala ya nane kama walivyoteuliwa.

clouds stream