Tuesday, 5 September 2017

Meya Chadema,Waziri Ummy Wazindua Bima Ya Afya Bure Kwa Wazee

Wazee mara baada ya kupata Bima ya  Afya.
Wazee mara baada ya kupata Bima ya Afya.
IMG-20170426-WA0006

Meya wa Ubungo Boniface Jacob pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu wamezindua huduma ya Bima ya Afya Bure kwa wazee wilaya ya Ubungo.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa vitambulisho vya wazee Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema utekelezaji wa matibabu bure kwa wazee ni wa lazima na siyo hiari kwakuwa serikali ya awamu ya tano imeweka sera zinazotekelezeka kwa kila hospitali za umma.

Mwalimu amezitaka Hospitali kubwa za rufaa kuweka taratibu maalumu za kuwasaidia wazee wenye kadi za bima ya afya ili kuhakikisha wanaokoa maisha yao.

Naye Mstahiki Meya wa Ubungo Boniface Jacob amesema gharama zilizotumika ni za mapato ya wilaya hiyo na sio mkopo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori amesema utekelezaji wa kutoa huduma kwa wazee kwa Manispaa hiyo kwa kufuata kadi hizo utazingatia weledi na haki ili kuondoa kero kwa wazee hao.

clouds stream