Friday, 8 September 2017

VIGOGO WALIOTAJWA SAKATA LA MADINI WATAKIWA KUJIUZULU

Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
IMG-20170426-WA0006

Rais Dkt.John Pombe Magufuli amewataka Vigogo wote wakiwemo Mawaziri aliowateua kujitathimini kufuatia kutajwa na Kamati mbili za Bunge zilizochunguza biashara ya madini ya Almasi na Tanzanite.

Rais Magufuli amesema hayo leo Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya kupokea ripoti mbili zilizoundwa na Spika wa Bunge Job Ndugai kuchunguza biashara ya madini ya Almasi na Tanzanite ambazo zimeibua uozo zikiwahusisha baadhi ya watendaji wa Serikali.

Vigogo hao ni waziri George Simbachawene ambaye kwa sasa ndiye Waziri katika Ofisi ya Rais Tamisemi ambaye alishawahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, anatajwa kuhusiana na biashara ya Tanzanite ambapo aliridhia mabadiliko katika mauzo ya kampuni uchimbaji Tanzanite na utoaji wa leseni kinyume na utaratibu.

Naibu Waziri Edwin Ngonyani naye ametajwa kuhusiana na kadhia ya kuzuia Serikali kununua mgodi wa almasi kwa dola milioni 10 na kuikosesha Serikali zaidi ya dola milioni 300, fedha ambazo zilienda kwa kampuni iliyonunua hisa.

Aidha kamati hiyo ilihoji namna ambavyo walioshiriki kukataa Serikali kununua mgodi huo wa almasi walivyopata bahati ya kuchaguliwa katika bodi ya waliouziwa hisa.

Kitendo cha Eliakim Maswi kusema kwamba alipatwa na hasira baada ya kutoka katika mgodi huo wa almasi na kujionea madudu na kuapa kutokanyaga tena kulielezwa na kamati hizo kuwa moja ya sababu ya watendaji kuacha mambo yakiharibika.

Aidha aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo ametajwa kupindisha mambo kadhaa na kufanya maamuzi bila kushirikisha bodi zinazotakiwa na hivyo kusababisha hasara kubwa.

Watu wengine waliotajwa katika taarifa zote mbili ni pamoja na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngereja, mwanasheria wa zamani George Werema Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) nalo limetajwa kuwa limeshindwa kusimamia Mikataba na Biashara ya Madini hivyo kupelekea Taifa kupata Hasara kubwa.

Mara baada ya kukabidhiwa Ripoti hizo Rais Magufuli naye amekabidhi kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili ziwakamate na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria vigogo hao.

Kwa mujibu Ushauri wa kamati Kwa upande wa kamati ya Dk Bitego iliyochunguza tanzanite imesema kuna haja ya kuwawajibisha wote waliohusika kuliingiza taifa hili katika mikataba mibovu isiyokuwa na tija na kuleta hasara.

clouds stream