Tuesday, 4 November 2014

JENGO LILILOSHAMBULIWA NA OSAMA BIN LADEN LAZINDULIWA

JENGO LILILOSHAMBULIWA NA OSAMA BIN LADEN LAZINDULIWA

Kituo cha One World Trade Centre chapita majengo yote katika mtaa wa Manhattan, jijini New York
Kituo cha One World Trade Centre chapita majengo yote katika mtaa wa Manhattan, jijini New York.
Miaka 13 baada ya majengo ya awali ya Kituo cha Biashara cha Kimataifa, WTO kuharibiwa katika shambulio la kigaidi likiongozwa na Osama Bin Laden la Septemba 11, 2001, kituo hicho kilichopo jijini New York kimefunguliwa kwa shughuli za biashara.
Jengo hilo lenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 3.8 limechukua muda miaka nane kulijenga na kwa sasa ndilo jengo refu kuliko yote nchini Marekani.
Jengo hilo lenye urefu wa mita 541 kwenda juu liko katikati ya eneo la New York, ikiwemo sehemu ya eneo la kumbukumbu la majengo ya zamani na makumbusho yaliyofunguliwa mwaka huu
Jengo hilo limekodishwa kwa asilimia 60% na taasisi ya serikali ya Marekani ya Utawala wa Huduma imeingia mkataba wa kuchukua eneo la futi za mraba 275,000.
“Mwonekano wa angani wa jiji la New York umerejea tena,” anasema Patrick Foye, mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Bandari, ambayo yanamiliki eneo hilo lililorejeshewa hali yake.

STYLE MPYA YA KUTOKA KIAFRIKA ZAIDI KUANZIA VIATU HADI POCHI ILIYOPAMBWA KWA KITENGE

  STYLE MPYA YA KUTOKA KIAFRIKA ZAIDI KUANZIA VIATU HADI POCHI ILIYOPAMBWA KWA KITENGE

Tarehe October 30, 2014
1385454_604011869640228_287566813_n1378613_602336346474447_349281641_n (1)1378015_603636296344452_408764044_n9314_618210831556511_49568873_n601511_629990030378591_194114663_n734792_512992942078301_763624956_n1001928_618211221556472_2075052068_n

ENTENTE SATIF MABINGWA WA AFRIKA 2014/15

ENTENTE SATIF MABINGWA WA AFRIKA 2014/15



Viongozi na wachezaji wa  Entente Satif wakishangilia ubingwa wao baada ya kuuchukua mbele ya AS VitaClub.
Viongozi na wachezaji wa Entente Satif wakishangilia ubingwa wao baada ya kuuchukua mbele ya AS VitaClub.
Klabu ya Entente Satif kutoka Algeria imeshinda ubingwa wa kilabu bora barani Afrika kwa mara ya kwanza katika miaka 26 baada ya kuishinda klabu ya AS Vita Club kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kutokana na mabao ya ugenini kufuatia sare ya 3-3 siku ya jumamosi.
Raundi ya pili ya fainali katika uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Blida ilikamilika kwa sare ya 1-1,siku sita baada ya sare ya 2-2 katika mechi ya kwanza iliochezwa mjini Kinshasa.
Setif ilianza kuona lango na wapinzani wao dakika nne katika kipindi cha pili kupitia Sofaine Younes ambaye alifunga bao kupitia pasi ya El Hadi Belameiri.
Lakini wageni hao walisawazisha dakika tano baadaye kupitia Lema mabidi aliyepiga mkwaju kutoka nje ya eneo la kupigia penalti ili kuimarisha matumaini ya timu yake.
Mabidi pia alikuwa ameifungia kilabu hiyo mabao yake mawili katika raundi ya kwanza ya mchuano huo wikendi iliopita.
Bao hilo lilisababisha mechi hiyo kuwa ngumu ambapo Vita ilionyesha mchezo mzuri ikilinganishwa na wapinzani wao Setif waliojaribu kutumia mbinu chafu za kupoteza mda huku mashabiki wa kilabu hiyo wakitaka mchezo huo kukamilishwa kuanzia dakika ya 75.

clouds stream