Friday, 4 March 2016

Saa Za Kisasa Zitumiwazo Kufanya Udanganyifu Katika Mitihani

Saa Za Kisasa Zitumiwazo Kufanya Udanganyifu Katika Mitihani

Tarehe March 4, 2016


160304101302_cheating_watch_640x360__nocredit
Saa za kisasa ambazo zimetengenezwa mahususi kutumiwa kudanganya wakati wa mtihani zimekuwa zikiwakosesha usingizi walimu na wasimamizi wa mitihani. Saa hizo zinatangazwa katika soko la kuuza bidhaa mtandaoni la Amazon.
Saa hizo zina uwezo wa kuweka akiba ya data na maelezo ambayo yanaweza kusomeka mtu anapofanya mtihani.
Aidha, zina kitufe cha dharura ambacho kinaweza kubadili uso wa saa hizo haraka sana na badala ya kuonesha kilichomo ndani ziwe zinaonesha uso wa kawaida wa saa.
Mojawapo ya aina ya saa hizo ina uwezo wa kuweka akiba data ya 4GB wakati  nyingine ambayo inatarajiwa kuanza kuuzwa baadaye mwaka huu  itakuwa na uwezo wa 8GB na inaweza kuhifadhi hata video.
Baadhi ya saa hizo  zina kifaa kidogo sana cha kusikilizia na hakitumii nyaya (wireless) jambo linalomwezesha mtu kusikiliza kilichohifadhiwa kwenye saa hiyo bila ya kuonekana.
Naibu Mwalimu Mkuu wa shule moja kutoka Bath, Uingereza anasema saa hizo zinaweza zikawashawishi wanafunzi kudanganya katika mtihani.
Amesema ingawa saa hizo zinaweza kudhibitiwa kwa kutumia sheria zinazoharamisha simu na kompyuta katika vyumba vya mitihani, bado ni changamoto kubwa sana kwa watu wanaosimamia mitihani hivyo uuzaji wa saa hizo unafaa kudhibitiwa.
Kuna pia “kalamu za kuiba mtihani” ambazo zinaweza kuhifadhi habari na maelezo.

Wednesday, 2 March 2016

Matokeo Mechi Za Jana EPL Na Msimamo Wa Ligi Angalia Hapa

Matokeo Mechi Za Jana EPL Na Msimamo Wa Ligi Angalia Hapa

Tarehe March 2, 2016
Kocha wa Manchester united Luis Van Gaal na Kocha wa Chelsea Guus Hiddink
Kocha wa Manchester united Luis Van Gaal na Kocha wa Chelsea Guus Hiddink

Tuesday 1st March 2016

 
BARCLAYS PREMIER LEAGUE
FIXTUREKICK-OFF
Aston Villa  1-3  EvertonFull time
Bournemouth   2-0   SouthamptonFull time
Leicester  2-2    West BromFull time
Norwich   1-2   ChelseaFull timet
Sunderland  2-2    Crystal PalaceFull time

 
POSITIONTEAMPLAYEDGOALDIFFERENCEPOINTS
No movement1Leicester282057
No movement2Tottenham272854
No movement3Arsenal271751
No movement4Man City262047
No movement5Man Utd271044
No movement6West Ham271043
No movement7Southampton28740
Moving up8Chelsea28439
Moving down9Stoke27-439
Moving up10Everton271338
Moving down11Liverpool26238
Moving down12Watford27137
No movement13West Brom28-736
No movement14Crystal Palace28-633
No movement15Bournemouth28-1232
No movement16Swansea27-1127
Moving up17Sunderland28-1924
Moving down18Norwich28-2224
Moving down19Newcastle26-2224

Sudani Kusini Yakubaliwa Uanachama Afrika Mashariki

Sudani Kusini Yakubaliwa Uanachama Afrika Mashariki

Tarehe March 2, 2016
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir.
Nchi ya Sudani leo imekubaliwa kujiunga na  Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC katika kikao kilicho ongozwa na Mwenyekiti wa sasa wa jumuia hiyo  Rais Dkt. John Magufuli wa Tanzania.
Sudan Kusini ilijitenga na Sudan tarehe 9 Julai mwaka uliopita ambapo ilituma maombi ya kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini jumuiya hiyo ilisema kwamba bado inakabiliwa na matatizo ya kisiasa na wala uchumi wake ambao asilimia 98 yake inategemea mauzo ya mafuta si wa kuridhisha.
Nchi  wanachama wa jumuiya hiyo  ni  Nairobi Kenya, Burundi, Rwanda, Uganda, Tanzania na Kenya.

clouds stream