
Asamoah Gyan akiifungia Ghana goli dakika za mwisho
Ghana wapata ushindi wa kwanza wa michuano ya mataifa ya Afrika baada
ya kupata ushindi wa 1-0 kwenye dakika za mwisho huku mwokozi akiwa
mchezaji aliyekosa mechi ya kwanza ya Ghana dhidi ya Senegal Asamoah
Gyan.Ushindi huo wa Ghana unainua matumaini ya kufuzu huku kundi hilo
likionekana bado lina ushindani mkubwa.Kwenye kundi C mpaka sasa Senegal
anaongoza baada ya kutoka sare na Afrika Kusini kwenye mechi iliyofuata
baada ya mechi ya Ghana kumalizika.

Black Stars walifanya mabadiliko mawili kwenye kikosi kilicholazwa 2-1
na Senegal, badiliko muhimu likiwa kureja kwa Asamoah Gyan safu ya
mashambulizi, na wakarejelea mpangilio wa 4-4-2.
Mbweha wa Fennec nao walifanya mabadiliko matatu kwenye kikosi
kilicholaza Afrika Kusini 3-1, Madjid Bougherra akiingia nafasi ya Rafik
Halliche ulinzi, na washambuliaji Saphir Taider na Ishak Belfodil
wakiingia.

Mechi hiyo ilionekana kana kwamba ingeisha sare, lakini dakika za
ushei mpira kutoka safu ya ulinzi ya Ghana ulimfikia Gyan na kwa ujanja
mkubwa na kasi akamlemea difenda Carl Medjani na kisha kumbwaga kipa
Rais Mbolhi na kufunga bao safi la ushindi.
Ghana XI: Brimah, Afful, Rahman, Amartey, Mensah, Acquah, A. Ayew, Badu, Atsu, Gyan, J. Ayew
Algeria XI: M’Bolhi, Mandi, Bougherra, Medjani, Ghoulam, Lacen, Taider, Bentaleb, Brahimi, Feghouli, Belfodi