Saturday, 24 January 2015

Gyan aiokoa Ghana, aipa pointi 3

Gyan aiokoa Ghana, aipa pointi 3


24FC80C600000578-0-image-a-46_1422036591690
Asamoah Gyan akiifungia Ghana goli dakika za mwisho
Ghana wapata ushindi wa kwanza wa michuano ya mataifa ya Afrika baada ya kupata ushindi wa 1-0 kwenye dakika za mwisho huku mwokozi akiwa mchezaji aliyekosa mechi ya kwanza ya Ghana dhidi ya Senegal Asamoah Gyan.Ushindi huo wa Ghana unainua matumaini ya kufuzu huku kundi hilo likionekana bado lina ushindani mkubwa.Kwenye kundi C mpaka sasa Senegal anaongoza baada ya kutoka sare na Afrika Kusini kwenye mechi iliyofuata baada ya mechi ya Ghana kumalizika.
24FC805B00000578-0-image-a-47_1422036608250
Black Stars walifanya mabadiliko mawili kwenye kikosi kilicholazwa 2-1 na Senegal, badiliko muhimu likiwa kureja kwa Asamoah Gyan safu ya mashambulizi, na wakarejelea mpangilio wa 4-4-2.
Mbweha wa Fennec nao walifanya mabadiliko matatu kwenye kikosi kilicholaza Afrika Kusini 3-1, Madjid Bougherra akiingia nafasi ya Rafik Halliche ulinzi, na washambuliaji Saphir Taider na Ishak Belfodil wakiingia.
24FC4F4100000578-0-image-a-26_1422034463036
Mechi hiyo ilionekana kana kwamba ingeisha sare, lakini dakika za ushei mpira kutoka safu ya ulinzi ya Ghana ulimfikia Gyan na kwa ujanja mkubwa na kasi akamlemea difenda Carl Medjani na kisha kumbwaga kipa Rais Mbolhi na kufunga bao safi la ushindi.
Ghana XI: Brimah, Afful, Rahman, Amartey, Mensah, Acquah, A. Ayew, Badu, Atsu, Gyan, J. Ayew
Algeria XI: M’Bolhi, Mandi, Bougherra, Medjani, Ghoulam, Lacen, Taider, Bentaleb, Brahimi, Feghouli, Belfodi

clouds stream