10. IM RICH (WHITE DIAMOND) $130.
Application hii nia yake tu ni kuonesha kua una hela. Haina kazi yoyote bali inajitokeza tu kwenye screen kuonesha kua una mahela ya kuchezea.
9. PC MAPPER $149.
Appliction hii ni kwaajili ya wasoma ramani na watu ambao wanafanya survey. Inatumika katika kutengenezea maeneo ya muhmu katika ramani na pia kuweza kurekebisha vitu mbalimbali katika ramani.
8. ANESTHESIA CENTRAL $149.95
Hii ni application ya kitabibu ambayo huongelea zaidi jinsi ya kufanya nusu kaputi. Huduma ya nusu kaputi ina pesa nyingi ila pia inaitaji uwezo mkubwa wa kitaalam na ndio maana application hii inauzwa bei.
7. NURSING CENTRAL $159.95
Application hii hutoa maelezo ya kutosha kwa wanafunzi na wanataaluma ya mambo ya unesi na pia husaidia katika huduma ya kwanza.
6. EMERGENCY CENTRAL $159.95
Hii huusika na huduma mbali mbali za kihospitali na mambo ya kidaktari zaidi.
5. MEDICAL CENTRAL $159.9
Medical central hutumika hasa kwa madaktari katika kuelezea mambo mapya na ya kali kuhusu taaluma zao na madawa mapya na ya zamani katika huduma za kidaktari.
4. MBE PREPARATIONS $199.99
Maandalizi ya mitihani ya bodi ni jambo la muhimu kwa wasomaji wengi. Sasa ukiwa mbali na vitabu na karibu na simu yako ukajiskia kusoma, chukua simu yako na usome ukiwa na apllication hii.
3. VUVUZELA WORLD CUP HORN PLUS $200
Kama umezimisi sana kelele za vuvuzela basi nunua application hii usikie hizo kelele. Pesa makaratasi aisee.
2. MOST EXPENSIVE PLAY APP $200
Hii haifanyi kitu chochote zaidi ya kukupa wallpaper ya kuonesha kua umenunua application ya bei ghali ila haisaidii lolote kwenye simu.
1. GOT CASH? $200
Application hii haina kazi yoyote zaidi tu ya kuonesha uwezo wako wa kununua chochote kwa pesa mingi. Haina kazi.