Monday, 19 May 2014

KUPUNGUZA UZITO, JE INAWEZEKANA?



Mtu anaweza kupungua kilo ngapi kwa wiki ni swali ambalo watu wengi hujiuliza.Hasa pale wanapotaka kuanza arakati za kupunguza uzito.Ni wazi kwamba watu wengi hupenda kufanya Dayati za muda mfupi na wapate matokea makubwa ya haraka.
Kiasi cha uzito unaoweza kupunguza kwa wiki hutofautiana kati ya mtu na mtu.Ingawa nia na juhudi binafsi huchukua nafasi kubwa katika hili,Kuna mambo engine  yanayoleta tofauti hizo
1.Jinsi
2.Umri
3.Ukubwa wa mwili
4.Vyakula unavyokula
5.Mazoezi unayofanya
Nguvu joto za chakula (calories)
Nguvu za chakula yaani kalori(kwa kiswahilli), calories (kwa kiingereza) ni kiasi cha nguvu ambacho hupatikana au hutolewa na chakula kifikapo mwilini.vyakula vyote (vyote viendavyo kinywani) vinaidadi fulani ya calories isipokua maji tu ambayo hayana calories.
Calories hufanya kazi mwilini kama ambavyo mafuta (petroli au dizeli) hufanya kazi kwenye gari.Ili gari iweze kutembea lazima mafuta yaungue ili kutoa nguvu ambayo hutumika kutembeza gari,na jinsi unavyozidi kutembea ndivyo ambavyo mafuta huzidi kuungua adi yanaisha
Mwili wa binadam nao hufanya vivyo hivyo,nguvu unazopata kwenye chakula yaani calories,huungua ili kutoa nguvu ambayo inauwezesha mwili wako kufanya mambo mbalimbali kuanzia kupumua,kutembea,kukimbia,na yote ambayo mwiili hufanya.Kadri unavyofanya shuguli nyingi zitumiazo nguvu ndivyo ambavyo calories hupungua mwilini.
Nusu kilo( 1/2 kg) ni sawa na calories 3500.Ili upunguze nusu kilo katika uzito wako nilazima utoe calories 3500 katika mwili wako.Unaweza kutoa  calories hizo katika mwili wako  kwa kupunguza kiasi cha calories unazokula kwa siku au kwakuongeza mazoezi au kufanya kazi zinazofanya utumie nguvu nyingi ili utumie nguvu za ziada ambazo mwili wako umetunza (unene wako)
Makala yakitafiti  iliyoandikwa na NBC NEWS mwaka 2009 ilisema kwamba ,kupunguza calories (chakula) ni muhim zaidi kuliko kufanya mazoezi hasa kwa mtu mwenyenia ya kupunguza uzito.Pia ilisema mtu hupunguza uzito kwa haraka zadi endapo atapunguza kiasi cha calories anazokula na kufanya mazoezi ya mwili ili kuunguza calories ambazo mwili wake umetunza.
Utofauti
Jins ya mtu huchangia katika kuamua ni kiasi gani cha uzito anaweza kupunguza kwa wiki..Kwa kawaida wanaume wanamisuli mingi kuliko wanawake.Tafiti za Mayo clinic ya marekani zinaonyesha kwamba misuli hutumia calories nyingi hivyo uwepo wake katika mwili hufanya mtu aweze kupunguza uzito kwaharaka.Hii hufanya wanaume waweze kupunguza mwili kwa haraka kuliko wanawake.
Pia tafiti hizo huonyesha kwamba mtu mwenye uzito mkubwa anauwezo wa kupunguza uzito kwa hararaka kuliko  mtu mwemye uzito mdogo,hasa mwanzoni anapoanza kupungua.
Mazoezi.
Kiasi cha calories unazoweza kutoa mwilini unapofanya zoezi au shughuli nyingine hutokana na uzito wamtu.Mtu mwenye uzito mdogo hutoa calories chache na mwenye uzito mkubwa hutoa calories nyingi kw akiasi kile kile cha mazoezi.
Mfano:mtu mwenye kilo 72.5 atatoa calories 986 kwa kukimbia kwa dakika 60,lakini mwenye kilo 108 atatoa calories 1,472 kwa kukimbia dakika hizo hizo 60
Kadri unavyotoa  calories nyingi mwilini ndivyo uzito unavyozidi kupungua
Dayati kali
Dayati kali hulenga kumfanya mtu apunguze uzito mwingi ndani ya muda mfupi.Tafiti huonyesha kwamba asilimia kubwa ya uzito unaopotea unapofanya dayati kali ni uzito wa maji mwilini.
Ni  ngumu sana kwa mwili kutoa kilo 1 ya mafuta mwilini kwa wiki.Hata ivyo endapo utaendelea na dayati kali kwa muda mrefu basi unaweza kupunguza mafuta ya mwili na hivyo kupunguza mwili kwa haraka.
Ukifanya dayati kali sana,ambayo inakufanya uingize calories chache sana mwilini basi kunauwezekano wa kupunguza kilo ndani ya muda mfupi.
Magonjwa na matibabu
Historia ya afya yako ni Sababu nyingine inayochangia katika kujua kiasi cha kilo unachoweza kupunguza kwa wiki.Magojwa yasababishwayo na homoni za mwili hufanya iwe ngumu sana kupunguza uzito wa mwili.

Tafiti zinaonyesha kwamba baadhi ya madawa kama madawa ya kisukari na dawa za uzazi wa mpango hufanya  iwe ngumu kupunguza uzito.Baadhi ya madawa pia hufanya mtu ashindwe kabisa kupunguza uzito na madawa mengine hunenepesha mwili.
Ushauri
Endapo umekua ukifanya mazoezi na dayati kwa muda mrefu na hupungui uzito,ni vyema ukamuaona Daktari wako na kumuelezea hali hiyo ili aweze kutafuta chanzo cha tatizo hilo na kulitafutia ufumbuzi.
Kama unafanya juhudi za kupunguza uzito basi punguza kiasi cha calories unazokula kwa siku na pia fanya mazoezi ili kuunguza calories za akiba mwilini.
Hitimisho.
Naamini umeelewa nikwanini hakuna kipimo maalum cha kiasi cha uzito ambao mtu anaweza kupunguza kwa wiki,kwani vigezo vyote hivi huchangia katika kupungua.
Hata ivyo vitu kama msongo wa mawazo na kutokupata usingizi wakutosha,pia huweza kuchangia mtu kupungua uzito au laa kuongeza uzito.
UNAWEZA KUPUNGUZA UZITO UKIAMUA ,HAIJALISHI UNAUZITO MKUBWA KIASI GANI


clouds stream