Tuesday, 20 May 2014

YAYA TOURE KUKASIRISHWA NA UONGOZI WA MANCITY.


City wamuudhi Toure
Wakala wa kiungo wa Machester City Yaya Toure amekashifu kupuuzwa kwa kiungo huyo kutoka Ivory Coast.
Dimitri Seluk alikashifu ujumbe wa kheri njema kwa Toure ambaye alikuwa anaadhimisha siku kuu ya kutimiza miaka 31 mnamo mei tarehe 13.

Ujumbe huo ulioambatana na keki haukumridhisha hata kidogo Seluk ambaye anasema kuwa alitarajia wamiliki wa klabu hicho angalau kumtambua kiungo huyo wa Ivory Coast ,timu hiyo ilipotua Abu Dhabi kusheherekea ushindi wao wa taji la Uingereza kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.
Seluk alisema Toure huenda akaondoka iwapo wamiliki wa klabu hiyo wataendelea kumpuuza.
Yaya Toure ameudhika Man City
Toure aliandikisha kandarasi mpya ya miaka minne mwaka uliopita licha ya Seluk ambaye amemuakilisha Toure kwa zaidi ya miaka kumi kutishia kuwa kiungo huyo wa Ivory Coast angehama Etihad.
Uhusiano baina ya mchezaji huyo bora barani Afrika na Seluk umedumu kwa miaka mingi kiasi ya kuwa Toure alimpa mwanawe wa pili jina la Seluk.

Dmitri Seluk

"'Itakuwaje siku ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya Roberto Carlos rais wa Anzhi alimnunulia gari aina ya Bugatti na eti bwenyenye mwenye Man city anatuma keki na ujumbe wa tweeter? Nilitarajia watamtambua hata kwa salamu tu lakini Iwapo hawatamheshimu basi huenda akaondoka Etihad "

clouds stream