Monday, 26 May 2014

BRAZUCA NDIO JIN RASMI LA KOMBE LA DUNIA BRAZIL.


Brazuca - mpira wa world cup
Brazuca ndilo jina la mpira rasmi utakaotumika katika mchuano wa kombe la dunia Brazil hapo 12 mwezi ujao.
Watengenezaji Adidas pamoja na baadhi ya wachezaji wameusifu kwa shabaha na wepesi.
Brazil kwenyewe ndiko kuna wasiwasi - na Gwiji wa soka nchini humo Pele anawahimiza raia wenzake warekebishe mambo. Balozi huyo wa soka mwenye umri wa miaka 73 Ametiwa wasiwasi na maandamano ya mara kwa mara ya kupinga matumizi ya hela nyingi za kuandaa kombe la dunia.
Maandamano hayo yameshangaza wengi kwani Brazil inahusudu na kusifika kwa ubingwa wao wa kusakata kandanda.

Ushauri

Pele anasihi maandamano hayo yakome kwani yatawafanya wapenzi wa kandanda wa ng'ambo waliokuwa wanauia kwenda kujionea mchuano huo kughairi.
Katika mkutano na waandishi habari huko Mexico amenukuliwa kusema, ana taarifa kuwa tayari 25%ya mashabikii wa kigeni wameshavunja safari zao za kwenda Brazil kwa sababu ya maandamano hayo na kama yakiendelea basi wengine wengi huenda wakakata safari hizo na hivyo kuleta hasara ya Brazil kukosa biashara hasa za kitalii.
Japo Pele anakubaliana nao katika maandamano hayo ya kutaka kuboreshwa kwa huduma za kijamii hasa za matibabu, usafiri na elimu, anasisitiza kuwa timu ya taifa ambayo imeiletea sifa tele nchi hiyo isitumiwe kulipia makosa ya ufisadi unaofanywa na wanasiasa ambao wanalaumiwa kwa maovu mengi ikiwemo kucheleweshwa kwa kukamilika kwa viwanja 12 vya mpira , huku kukiwa zimesalia takriban wiki 3 tu kabla kombe hilo kuanza.
Brazil ikiwa ndilo taifa lililoshinda kombe la dunia mara nyingi kuliko lengine tena ugenini inakumbwa na shinikizo kubwa la kushinda kombe hilo nyumbani.

Maandalizi

Kufikia sasa ni nchi chache tu ambazo tayari zimetaja vikosi vyao ikiwemo hiyo Brazil na Uingereza, ambako, nahodha wa timu hiyo Steven Gerald nae amekuwa akitathmini jinsi kikosi cha timu ya taifa lake kilivyo na wachezaji chipukizi kiasi cha kuogofya.
Anasema anatumaini kuwa hawatashikwa na mchecheta wa uoga watakapokuwa uwanjani Brazil. Majina yanayotajwa sana katika timu hiyo ya Uingereza ni akina Ross Barkley, Raheem Sterling na Luke Shaw. Nahodha Gerrard amewaomba wachezaji waliokomaa pamoja na yeye mwenyewe wawashauri vyema vijana hao chipukizi watakapokuwa huko safarini kutafuta ubingwa wa dunia katika soka.
Mechi ya kwanza ya Uingereza watakumbana na wa-italaino hapo juni 15 katika uwanja ulioko eneo la msitu wa nyika ya Amazon kunakojulikana kuwa na joto si haba.
Nasi hapa kikosi cha BBC michezo tukapopasha kila joto hilo la kombe la dunia litakavyokuwa linapanda, huku Afrika tukiwakilishwa na Aljeria , Nigeria, Ghana, Cameroon na IVORY Coast .

clouds stream