Sunday 11 May 2014

JESHI LA NIGERIA LILIPUUZIA ONYO JUU YA BOKO HARAM


Jeshi la Nigeria lilipata onyo la mapema kuhusu utekaji nyara wa wasichana 270, lakini likakosa kuchukua hatua zozote.
Taarifa hii ni ni kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International.
Shirika hilo linasema kuwa lina taarifa za kutosha kutoka kwa watu mbali mbali kuwa jeshi lilipewa onyo la kundi la Boko Haram kuhusu mpango wao wa kuwateka nyara wanafunzi hao.
Wasichana 53 waliweza kutoroka kutoka mikononi mwa Boko Haram na kuwaacha wasichana wengine 200 wakiwa mateka.
Maafisa wa serikali bado hawajatoa tamko lolote kuhusu madai ya Amnesty. Wakati huohuo Boko Haram wamesema kuwa watawauza wasichana hao.
Boko Haram wamekiri kuwateka nyara wasichana hao wakisma kuwa hawapaswi kuwa shuleni wakisoma bali wanapaswa kuolewa na kuwa wake wa watu.
'Wataalamu wa kijeshi'
Kadhalika shirika la Amnesty linasema licha ya onyo kutoka kwa Boko Haram , jeshi halikuchua hatua zozote kuzuia tukio hilo la utekaji nayar aktika kijiji cha Chibok.
Shirika hilo linasema kuwa kulikuwa na wasiwasi wa jeshi kupigana na kundi la Boko Haram ambalo linaonekana kuwa na zana nzito kuliko jeshi.
Inaaminika kuwa wasichana hao wamezuiliwa katika msitu mkubwa kutoka Chibok ambako wasichana wlaitekwa nyara hadi katika eneo la mpaka na Cameroon.
Watalaamu wa kijeshi kutoka Marekani na Uingereza wamwasili nchini Nigeria kujaribu kuwatafuta wasichana hao ili kuwaokoa.
Kundi hilo limekuwa likipinga elimu ya kimagharibi tangu kuanza harakati zake katika jimbo la Borno mwaka 2009.
Takriban watu 1,200 wanaaminika kuuawa katika ghasia zilizosababishwa na kundi hilo mwaka huu pekee.

clouds stream