Manchester City ndio mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu.
Vijana wa Manuel Pelligrini walitawazwa mabingwa katika siku ya mwisho ya ligi kuu ya Uingereza baada ya kuilaza West Ham mabao 2-0.Umati uliojaa uwanjani Etihad ulimiminika uwanjani baada ya kipenga cha mwisho.Samir Nasri nahodha Vincent Kompany ndio waliomhakikishia Pelleigrini alama tatu muhimu zilizotosha kuipiku Liverpool iliyomaliza katika nafasi ya pili alama 86 mbili nyuma ya City ambao wametwaa taji lao la pili katika kipindi cha miaka mitatu.
Kocha huyo kutoka Chile alifaidika na kichapo cha Liverpool mikononi mwa Chelsea na hivyo alihitaji sare ya aina yeyote kujihakikishia ushindi.
Mancity iliititima West ham 2-0 na kutamatisha msururu wa mechi tano bila ya kushindwa .
Pelligrini, atakumbukwa kwa kuirejesha kombe Etihad baada ya Roberto Mancini kupigwa kalamu kwa kushindwa kutetea taji msimu uliopita .
Kocha huyo mwenye miaka 60 anajivunia mabao 102.
Kwa upande wao Liverpool walisajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Newcastle United uwanjani Anfield.