Tuesday, 25 November 2014

HOUSES FOR SALE



House for sale:Amoderm house for sale it is a South African brick made ( interlocking bricks )  house, with 3 spacious master bed rooms for sale. LOCATION: Boko kwa mwamba, SIZE: Block fence zqm 420, TITTLE: 3 years ( no loan, smart ), PRICE: tsh. 125 mill ( semifinished ) and tsh. 150 mill (finished).Morgage acceptable



House for sale: 5 bed rooms house located near Kinyerezi catholic church. Has spascious 5 bed rooms, kithcen, dinning / sitting room, SIZE: 400 sqm , no titttle, PRICE: tsh.120 mill ( negotiable )




HOUSE FOR SALE: A house with huge compound full of trees, located at Kibamba ccm, near Kibamba primary school, 1750 sqm ( two plots ) . PRICE: tsh. 170 mill, tittle 99 years also it has home morgage loan in bank.
HOUSE FOR SALE: we have a new 3 bed rooms house at Kinyerezi ( Tabata ) for sale, have a block fence, no tittle. PRICE: tsh. 60 mill
HOUSE FOR SALE: Stone buiding for sale located at Sinza kijiweni, 3 apartment semi finished, 250 sqm with title, price; tsh. 800 mill (negotiable).
HOUSE FOR SALE: A house located at Mbezi Msigani, 4 bed rooms, kitchen,sitting or dinning room has a title deed, price:tsh 50 mil (installment allowed).

Sunday, 23 November 2014

WENGER ALIA NA MABEKI KIPIGO CHA MAN U

WENGER ALIA NA MABEKI KIPIGO CHA MAN U


Kocha wa arsenal Arsene Wenger amewalaumu walinzi wa timu hiyo kufuatia ushindi wa manchester United.
Kocha wa arsenal Arsene Wenger amewalaumu walinzi wa timu hiyo kufuatia ushindi wa manchester United.
Mkufunzi wa Arsenal Arsene wenger amesema kuwa safu ya ulinzi ya Arsenal ni hafifu baada ya kushindwa 2-1 na Manchester United katika uwanja wa Emirates.
Arsenal walipatikana wakiwa wazi katika safu ya nyuma walipojaribu kutafuta bao la kukomboa baada ya Kieran Gibs kujifunga.
Wenger amesema kuwa kwa sasa safu hiyo ya ulinzi haina uzoefu wa kutosha kuweza kusoma mechi.
Katika mechi hiyo Arsenal walifanya mashambulizi 23 katika lango la Manchester United.
Wenger aliongezea ”ni mechi tuliotawala kwa asilimia 80 na hatujatawala mechi kama hivo kwa mda mrefu”.
”Mwisho wa mechi hatukuwa imara katika safu ya Ulinzi na tulifanya makosa ambayo walichukua fursa na kutuadhibu”.

SAKATA LA ESCROW: WALIOGAWANA FEDHA ZA UMMA KUJULIKANA WIKI HII


SAKATA LA ESCROW: WALIOGAWANA FEDHA ZA UMMA KUJULIKANA WIKI HII



Wabunge kujadili wizi mabilioni ya fedha za umma wiki hii mjini Dodoma.
Wabunge kujadili wizi mabilioni ya fedha za umma wiki hii mjini Dodoma.
Sakata la wizi wa mabilioni ya fedha za umma katika akaunti ya Escrow watuhumiwa wote kujulikana wiki hii siku ya jumatano na Alhamisi. Katika siku hizo Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania linatarajia kujadili ripoti ya escrow.
Hivi sasa  Wabunge wa kila vyama wamekuwa wakikutana kuweka misimamo yao kuhusu namna watakavyoshiriki kujadili ripoti hiyo ili kuokoa mabilioni ya fedha za wananchi zilizoibwa na watendaji wa serikalini na hatimaye kugawana.
Aidha,  katika Kikao cha Kamati ya Uongozi  wa Bunge  kilichofanyika jana asubuhi kilikubaliana suala hilo la escrow lijadiliwe kwa siku mbili badala ya moja  kama  iliyokuwa imepangwa awali.
Kwa upande mwingine   kambi Rasmi ya Upinzan Bungeni, imeibuka na madai kwamba  vigogo wanaotuhumiwa  kugawana fedha  za Escrow   wamenyofoa   baadhi ya karatasi zenye majina yao  ili kuficha  ushaidi  ambapo  wameandaa   propaganda ya kuwahadaa wananchi kuwa ripoti hiyo haijakamilika.
Naye Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia ametaja kurasa zilizonyofolewa katika ripoti hiyo kuwa ni zilizobeba mambo ya msingi ambazo ni ukurasa wa 57, 58 na 59.
Watanzania wanausubiri kwa hamu kubwa mjadala huo utakaorindima wiki hii ili kuwafahamu walioiba fedha za umma na kugawana huku mambo ya msingi kama ujenzi wa shule, madawa hospitalini yakikwama kutokana na tamaa ya watu wachache wasio wazalendo.

KENYA: MAUAJI WATU 28 YAHUSISHWA NA VITA YA KIDINI


KENYA: MAUAJI WATU 28 YAHUSISHWA NA VITA YA KIDINI



Mauaji yaliyotokea nchini Kenya yadaiwa kuwa ya kulipiza kisasi.
Mauaji yaliyotokea nchini Kenya yadaiwa kuwa ya kulipiza kisasi.
Mshauri wa ngazi ya juu wa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa mauaji ya watu 28 waliokuwa wakisafiri kwenye basi moja yalilenga kusababisha vita vya kidini nchini kenya.
Aidha.Bw Abdikadir Mohammed alitoa wito kwa wakenya kutoka imani zote kuungana pamoja dhidi ya kile alichokitaja kuwa vitendo vya uhalifu.
Katika tukio la mauaji ya  watu 28 ambapo  wapiganaji  wa kundi la Al-Shabaab waliwapiga risasi wasafiri  ambao  hawangeweza   kukariri Koran.
Al Shabaab ilisema kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kulipiza kisasi mauji ya hivi majuzi ya waislamu yaliofanywa na wanajeshi wa Kenya kwenye mji wa pwani ya Mombasa.
Serikali ya Kenya imesema kuwa imeanza kuwatambua waliotekeleza mauaji hayo na itawafikisha mbele ya sheria hivi karibuni.

Friday, 14 November 2014

PROPERTIES FOR SALE AND RENT





HOUSE FOR SALE: semi finished at Kinondoni, 3 bed rooms one being a master, spacious sitting room,dinning and kitchen, price is tsh. 300 -250 mill.
PROPERTIES FOR SALE: propertis for sale are available at a cheap and negotiable price, 3 bed rooms, spacious sitting/ dinning,kitchen and store, fanced with block and a modern gate LOCATION: few metres from kinyerezi catholic church, has a nice neighbour hood PRICE: tsh 60 mill negotiable. No tittle yet, SIZE: 650 sqm.
HOUSE FOR SALE:A moderm 3 bedrooms, a master, dinning/ sitting and kithen, no fance yet, near catholic church, PRICE: tsh. 100 mill, no tittle deed.
YARD FOR SALE: located at Mikocheni industrial area, SIZE:6860 sqm, PRICE: 1.4 bill negotiable.
YARD FOR RENT: It is located at Mabibo opposite with Loyola secondary school, PRICE: tsh. 700000 per month.

Monday, 10 November 2014

RAIS KIKWETE AFANYIWA UPASUAJI TEZI DUME

RAIS KIKWETE AFANYIWA UPASUAJI TEZI DUME


Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Hospital ya
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Hospital ya Johns Hopkins nchini Marekani.
Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amefanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania, Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.
Upasuaji huo ulikuchukua kiasi cha saa moja  na nusu ambapo inaelezwa kuwa umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa.
Taarifa hiyo inasema hali ya Rais Kikwete anaendelea vizuri japo bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.

ARSENAL YAKUBALI KIPIGO

ARSENAL YAKUBALI KIPIGO


1415555713459_wps_10_Swansea_City_s_Bafetimbi_
Magoli mawili ya Swansea city yalio fungwa dakika ya 75 na 78 yameizamisha Arsenal na kuitupa mpaka nafasi ya 6 kwenye msimamo wa Ligi kuu nchini Uingereza.Goli la Arsenal limepachikwa na mchezaji aliye kwenye kiwango chake kwa sasa Alex Sanchez kwenye dakika ya 63.Kocha wa Arsenal,Arsene Wenger akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa Habari amesema timu yake inakabiliwa na majeruhi kibao ndio maana inashindwa kuikabili misukosuko ya Ligi na mpaka mwisho wa mchezo Swansea 2-1 Arsenal.Mechi nyingine zilizochezwa jana na matokeo yake Tottenham 1-2 Stoke, Sunderland 1-1 Everton, Westbrom 0-2 Newcastle.
1415553372955_wps_81_Arsenal_goalkeeper_Wojcie
Wachezaji wa Swansea wakilipa misukosuko lango la Arsenal
1415554549807_wps_87_Arsenal_s_Chilean_striker
Alex Sanchez akiifungia Arsenal goli kwenye dakika ya 63

DK MUNROE NA MKEWE WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA NDEGE

DK MUNROE NA MKEWE WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA NDEGE



munroe
Dr. Myles Munroe akiwa na mkewe Ruth enzi za Uhai wao
Rais wa MMI Bingwa wa Masuala ya Utawala na Uongozi kutoka Bahamas ambaye anajulikana sana kwa jina la Dr. Myles Munroe amefariki dunia pamoja na mkewe Ruth na mtoto wao wa kike kwenye ajali ya ndege iliyotokea huko Grand Bahama jumapili jioni.Katika ajali hiyo, ndege ndogo waliyokuwa wakisafiria iligonga winchi na kulipuka wakati ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Grand Bahama.

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA JESHI LA POLISI 2014

 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA JESHI    LA POLISI 2014

Tarehe November 10, 2014
Wanafunzi wa mafunzo ya upolisi katika moja ya vyuo vya mafunzo ya Polisi nchini Tanzania.
Wanafunzi wa mafunzo ya upolisi katika moja ya vyuo vya mafunzo ya Polisi nchini Tanzania.
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa majina ya wanafunzi wa kidato cha nne  mwaka 2013 na cha sita mwaka 2014. Angalia hapa umechaguliwa kwenda chuo kipi cha mafunzo ya Polisi.
Maelekezo Muhimu.
  1. Wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2014, kidato cha nne mwaka 2013 na JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo, Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea, Mbweni, Maramba, Chita, Makutupola, Mtabila, Msange, Mgulani, Oljoro, Rwankoma na Kimbiji wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi.
  2. Wahitimu hawa waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti tarehe 28/11/2014 kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa kama ilivyooneshwa kwenye jedwali hapa chini ili waandaliwe usafiri wa kuwapeleka Shule ya Polisi Tanzania tarehe 30/11/2014.
  3. Zoezi la usajili litaanza shuleni hapo tarehe 01/12/2014 hadi tarehe 15/12/2014. Atakaefika kuanzia tarehe 16/12/2014 hatapokelewa.
  4. Atakaeamua kuripoti kwa Kamanda wa Polisi ambako hakupangiwa atalazimika kujigharimia usafiri hadi Shule ya Polisi Tanzania mjini Moshi.
  5. Vijana hawa watalazimika kufika shuleni wakiwa na mahitaji yafuatayo:
    1. Vyeti vyao vyote vya masomo( original Academic Certificates/Result slip pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa (Original Birth certificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
    2. Mashuka mawili rangi ya Bluu Bahari (light blue)
    3. Chandarua chenye upana futi tatu
    4. Nguo za michezo(Track suit nyeusi,Tshirt blue na Raba)
    5. Pasi ya Mkaa
    6. Ndoo moja
    7. Pesa za kulipia bima ya afya kiasi cha shilingi elfu hamsini na mia nne tu (50,400/=).
    8. Pesa kidogo ya kujikimu.
  6. Kwa mujibu wa kanuni za shule ya Polisi ni marufuku kufika shuleni na simu ya mkononi. Atakayepatikana na simu atafukuzwa shuleni hapo. Shule itaelekeza na kusaidia kufanya mawasiliano.

Wednesday, 5 November 2014

CAVANI AIBEBA PSG IKISHINDA1-0

CAVANI AIBEBA PSG IKIPIGA MTU 1-0



Edenson Cavani akiifungia PSG bao muhimu katika ushindi wa 1-0 hapo jana katika mchezo wa klabu bingwa Ulaya.
Edenson Cavani akiifungia PSG bao muhimu katika ushindi wa 1-0 hapo jana katika mchezo wa klabu bingwa Ulaya.
Klabu ya PSG kutoka Ufaransa jana imeitungua Apoel Nicosia kwa bao 1-0 katika michuano ya klabu bingwa Ulaya michezo iliyopigwa jana.
Shukrani kwake mshambuliaji wa PSG Edenson Cavani ambaye alipiga bao hilo pekee kwa kuunganisha kroi kwa kichwa cha kuogerea.

RAIS WA SUDAN KUSINI AANGUKA UWANJA WA NDEGE

RAIS WA SUDAN KUSINI AANGUKA UWANJA WA NDEGE


Sudan's First Vice President Mayardit meets Darfur chief mediator Bassole and Qatar's Foreign Minister Ahmed in Juba in south Sudan

Katika hali isiyotegemewa Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ameanguka chini muda mfupi baada ya kuwasili kwenye mji mkuu wa Sudan,Khartoum kukutana na Rais wa Sudan Omar al Bashir,baada ya tukio hilo maafisa wa Ulinzi wa Rais Salva Kiir waliamuru kwa nguvu mwandishi aliyepiga picha ya tukio hilo azifute mara moja ili kuondoa ushahidi wa tukio hilo.Watu walifuatilia tukio hilo wanasema chanzo cha Rais Salva Kiir kuanguka ni kuchoka,pia baada ya madaktari kufanya uchunguzin aliondoka na gari uwanja wa ndege

KIWANGO CHA UFAULU CHAPANDA MATOKEO YA DARASA LA SABA

KIWANGO CHA UFAULU CHAPANDA MATOKEO YA DARASA LA SABA


MITIHANI YA DARASA LA SABA MORO

Baraza la Mitihani la Taifa  (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba yanayoonyesha kuongezeka kwa ufaulu. Kanda ya ziwa yafanya vizuri zaidi.

KISA FREEMASON MZEE WA UPAKO AMIMINA RISASI MTAANI

KISA FREEMASON MZEE WA UPAKO AMIMINA RISASI MTAANI

.

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar,  Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ usiku wa kuamkia Jumatatu iliyopita  alizua la kuzua kufuatia kumimina risasi kadhaa hadharani kwa madai ya kuwatawanya kundi la vijana waliodaiwa kumvamia na kuziba barabara kwa lengo la kumfanyia kitu mbaya. 
 Ishu hiyo iliyojaa utata mkubwa, ilitokea saa nne usiku maeneo ya Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam kwenye barabara inayotoka barabara kuu kwenda kanisani kwake.
MAELEZO YA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, tukio lilianza kwa Mzee wa Upako aliyekuwa akipita kwa miguu kukejeliwa na vijana waliomwita Freemason kauli ambayo mtumishi huyo wa Mungu aliiona ni ya kejeli kwake.“Baada ya kuitwa Freemason, yule kijana akiwa na wenzake waliendelea kumkejeli Mzee wa Upako, akawafuata na kuwauliza mbona mnanitukana, nimewakosea nini?”
RISASI ZARINDIMA
“Alipoona wale vijana wanazidi kumkejeli huku wakionesha dalili za kumfanyia fujo ndipo alipotoa bastola yake na kufyatua risasi tatu juu hali iliyowafanya wale vijana kutawanyika huku na kule.
“Baadhi ya watu walikuwa kwenye biashara zao, nao walitimua mbio, wengine waliacha biashara, unajua risasi ni risasi tu, mtu akisikia risasi hawezi kukaa salama hata kama ni mjeshi,” kilisema chanzo hicho.
Moja wapo ya alama zinazoaminiwa kuwa ni za Freemasons
MZEE WA UPAKO ATIMUA MBIO
Ilizidi kudaiwa kwamba, kufuatia kimbiakimbia hiyo, Mzee wa Upako naye alikimbia. Baadaye alirudi eneo la tukio kimachale na kukuta watu wameanza kukusanyika kujua kulikoni.“Mzee wa Upako alipofika aliagiza mtu atakayeokota ‘magazini’ ya risasi alizofyatua angempa shilingi alfu ishirini, vijana wengine wakaingia kazini, wakapata moja, wakapewa chao, Mzee wa Upako akasema mtu akiokota nyingine aipeleke polisi,” kilisema chanzo.
MADAI YA WATU
Kuna madai kwamba, vurugu hizo zilipambwa na kijana mmoja anayeitwa Robert ambapo mtumishi huyo wa Mungu alimkomalia kuwa ndiye aliyekuwa akiongoza wenzake kumtukana na kumkashifu kwamba yeye ni Freemason na si mchungaji wa kiroho kama anavyojiita.
MZEE WA UPAKO NA GAZETI LA AMANI
Kufuatia madai hayo, gazeti hili lilimtafuta Mzee wa Upako kwa njia ya simu na alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alikiri kutokea na kueleza ‘full’ mkanda.“Ni kweli lilitokea. Ni kwamba, siku hiyo nilipofika eneo lile kuna vijana wa kihuni walinifuata kwa nyuma, wakaanza kupigapiga gari langu, wengine wakizuia njia huku wakidai eti mimi ni Freemason.
Mfano wa silaha ya moto (bastola) kama  ile ya Mzee wa Upako.
“Nilijaribu kuwaambia kwamba mimi ni kiongozi wa kiroho lakini badala yake wakaanza kuniangushia matusi. Ili kujiokoa nilifyatua risasi hewani kuwatawanya,” alisema Mzee wa Upako.
Alipoulizwa kama anaweza kujua sababu za watu hao kumvamia na kumwambia yeye ni Freemason, kiongozi huyo alisema:
“Siwezi kujua, lakini mara baada ya kufyatua risasi na wao kutawanyika mimi niliamua mwenyewe kwenda Kituo cha Polisi Urafiki (Dar) kutoa taarifa.“Mimi siwezi kujua sababu za watu hao kunikashifu na kunitukana labda ukiwapata watakuambia lakini ni watu ambao naamini wametumwa na mtu f’lani ambaye mimi siwezi kukwambia lakini polisi watamjua baada ya upelelezi wao,” alisema.
Alipoulizwa alikuwa anatoka wapi usiku huo, Mzee wa Upako akajibu kwamba alikuwa anawenda kanisani kwake Ubungo Kibangu kwenye shughuli zake za kawaida za kiroho.
MADAI YA ROBERT
Madai ya upande wa Robert anayedaiwa kuongoza vijana wenzake kumfanyia vurugu Mzee wa Upako yanasema kuwa, baada ya mtiti huo wa risasi, yeye alikimbilia Kituo cha Polisi Mbezi, Dar na kufungua malalamiko yenye Kumbukumbu Na. JMD/RB/11099/2014 KUTISHIA KUUA KWA RISASI!Hata hivyo, Robert alipopigiwa simu ili kuulizwa kwa undani hakupokea  licha ya kuita kwa muda mrefu na kutumiwa meseji kwa namba yake ya simu.

Tuesday, 4 November 2014

RAIS WA UKRAINE APINGA UCHAGUZI

RAIS WA UKRAINE APINGA UCHAGUZI


Rais Petro Poroshenko wa Ukraine apinga kufanyika uchaguzi katika eneo lenye machafuko.
Rais Petro Poroshenko wa Ukraine apinga kufanyika uchaguzi katika eneo lenye machafuko.
Rais Petro Poroshenko wa Ukraine amesema kuwa hatambui uchaguzi unaoendelea katika baadhi ya maeneo ya Mashariki mwa nchi hiyo na kwamba kwa hatua hiyo wanarudisha nyuma jitihada za kuleta amani nchini humo.
Katika hotuba yake iliyoonyeshwa kwenye Runinga pia Poroshenko amesema kuwa serikali yake haitatambua upigaji kura huo katika majimbo ya Donetsk and Luhansk kutokana na kuwepo machafuko hivyo kukosekana amani.
Hata hivyo amesema kuwa hali ya machafuko katika mashariki mwa taifa hilo kumesababisha kuvunjika kwa hali ya amani na kuleta vurugu.
Katika hatua nyingine, Poroshenko amesema kuwa anatarajia kupendekeza sheria itakayopiga marufuku waasi  katika eneo ambalo limepitishwa na kuwa eneo lenye harakati za kutaka kuleta amani.

JENGO LILILOSHAMBULIWA NA OSAMA BIN LADEN LAZINDULIWA

JENGO LILILOSHAMBULIWA NA OSAMA BIN LADEN LAZINDULIWA

Kituo cha One World Trade Centre chapita majengo yote katika mtaa wa Manhattan, jijini New York
Kituo cha One World Trade Centre chapita majengo yote katika mtaa wa Manhattan, jijini New York.
Miaka 13 baada ya majengo ya awali ya Kituo cha Biashara cha Kimataifa, WTO kuharibiwa katika shambulio la kigaidi likiongozwa na Osama Bin Laden la Septemba 11, 2001, kituo hicho kilichopo jijini New York kimefunguliwa kwa shughuli za biashara.
Jengo hilo lenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 3.8 limechukua muda miaka nane kulijenga na kwa sasa ndilo jengo refu kuliko yote nchini Marekani.
Jengo hilo lenye urefu wa mita 541 kwenda juu liko katikati ya eneo la New York, ikiwemo sehemu ya eneo la kumbukumbu la majengo ya zamani na makumbusho yaliyofunguliwa mwaka huu
Jengo hilo limekodishwa kwa asilimia 60% na taasisi ya serikali ya Marekani ya Utawala wa Huduma imeingia mkataba wa kuchukua eneo la futi za mraba 275,000.
“Mwonekano wa angani wa jiji la New York umerejea tena,” anasema Patrick Foye, mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Bandari, ambayo yanamiliki eneo hilo lililorejeshewa hali yake.

STYLE MPYA YA KUTOKA KIAFRIKA ZAIDI KUANZIA VIATU HADI POCHI ILIYOPAMBWA KWA KITENGE

  STYLE MPYA YA KUTOKA KIAFRIKA ZAIDI KUANZIA VIATU HADI POCHI ILIYOPAMBWA KWA KITENGE

Tarehe October 30, 2014
1385454_604011869640228_287566813_n1378613_602336346474447_349281641_n (1)1378015_603636296344452_408764044_n9314_618210831556511_49568873_n601511_629990030378591_194114663_n734792_512992942078301_763624956_n1001928_618211221556472_2075052068_n

ENTENTE SATIF MABINGWA WA AFRIKA 2014/15

ENTENTE SATIF MABINGWA WA AFRIKA 2014/15



Viongozi na wachezaji wa  Entente Satif wakishangilia ubingwa wao baada ya kuuchukua mbele ya AS VitaClub.
Viongozi na wachezaji wa Entente Satif wakishangilia ubingwa wao baada ya kuuchukua mbele ya AS VitaClub.
Klabu ya Entente Satif kutoka Algeria imeshinda ubingwa wa kilabu bora barani Afrika kwa mara ya kwanza katika miaka 26 baada ya kuishinda klabu ya AS Vita Club kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kutokana na mabao ya ugenini kufuatia sare ya 3-3 siku ya jumamosi.
Raundi ya pili ya fainali katika uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Blida ilikamilika kwa sare ya 1-1,siku sita baada ya sare ya 2-2 katika mechi ya kwanza iliochezwa mjini Kinshasa.
Setif ilianza kuona lango na wapinzani wao dakika nne katika kipindi cha pili kupitia Sofaine Younes ambaye alifunga bao kupitia pasi ya El Hadi Belameiri.
Lakini wageni hao walisawazisha dakika tano baadaye kupitia Lema mabidi aliyepiga mkwaju kutoka nje ya eneo la kupigia penalti ili kuimarisha matumaini ya timu yake.
Mabidi pia alikuwa ameifungia kilabu hiyo mabao yake mawili katika raundi ya kwanza ya mchuano huo wikendi iliopita.
Bao hilo lilisababisha mechi hiyo kuwa ngumu ambapo Vita ilionyesha mchezo mzuri ikilinganishwa na wapinzani wao Setif waliojaribu kutumia mbinu chafu za kupoteza mda huku mashabiki wa kilabu hiyo wakitaka mchezo huo kukamilishwa kuanzia dakika ya 75.

clouds stream