Tarehe
July 19, 2015
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa.
Madiwani 20 wa Chama Cha Mapinduzi CCM katika Jimbo la Monduli,
wamejiunga na Chadema kufuatia Mbunge wa jimbo hilo Edward Lowassa jina
lake kukatwa wakati akiomba ridhaa ya kugombea urais kupitia chama
hicho.
Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara kiongozi wa Madiwani hao,
Julius Kalanga kutoka Kata ya Lepurko ambaye pia alikabidhi kadi yake
na za wenzake 19 wa CCM kwa viongozi wa Chadema huku wakisisitiza kuwa
wamefanya uamuzi mgumu ambao Lowassa amekuwa akiusema mara kwa mara
katika safari yake ya siasa.
Madiwani waliohama kutoka chama cha Mapinduzi kwenda Chadema
Madiwani waliohama chama ni Kalanga mwenyewe, Edward Lenanu, Bazir
Siamini, Sigur Olekibinti, Loti Yamat, Goodluck Lerunya, Pashet
Sengurumi, Yase Runja, Gidion Kimongishu, Dora Kipuyo, Mary Morindat,
Sara Lomayan na Halima Lusinde.
Kata ya Engaruka, Engutoto, Esilalei, Loksale, Majengo, Makuyuni,
Meserani, Nalalani, Lemooti, Moita, Monduli Juu, Monduli Mjini,
Mferejini, Mswakini, Mto wa Mbu, Migungani, Selela, Sepeko na Lashaini.
Dotto Mlacha, Hawa Nyambiry, Alex Kamanda, Sion Kapela, Maria Lemta,
Onesmo Naikoyo, Shaban Adam, Enditosidai Naikulo na Elifuraha Simon.
Wengine ni Dinna Solomon, Loti Naparana, Jocy Laizer, Edward Mathayo,
Piniel Loning’o, Napir Mukare, Inot Leringa, Kalaine Lowassa, Maria
Mepukori, Mary Stivin na Edward Kone.
Katika hatua nyingine, tangia kukatwa jina lake Mbunge huyo
hajazungumza jambo lolote ambapo alitaka kuzungumza na waandishi wa
habari nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam hata hivyo mkutano huo
uli ahirishwa kwa madai kwamba amechelewa kuwasili jijini Dar es salaam
akitokea mkoani Dodoma.