Monday, 31 August 2015

Maelfu wajitokeza Ukawa wakizindua Kampeni

Maelfu wajitokeza Ukawa wakizindua Kampeni


Wagombea Urais wa UKAWA Edward Lowassa na Juma Duni Haji.
Maelfu ya wananchi  ya wananchi wamejitokeza katika uwanja wa Jangwani leo jijini Dar es salaam kushuhudia uzinduzi wa Kampeni za Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Uzinduzi huo umekuwa wa aina yake kufuatia kuwa na shamra shamra nyingi na za aina yake kuanzia jana siku ya ijumaa ambapo inadaiwa baadhi ya wananchi walilazimika kulala katika viwanja vya Jangwani kusubiri uzinduzi huo.
Akizungumza  katika mkutano huo  Mwenyekiti wa Chadema Freeman  Mbowe amesema kwamba wamezindua kampeni zao leo ili kuhakikisha kuwa wanawapa wananchi mabadiliko wanayo yataka ambayo yataleta maisha mapya kwa watanzania.
Amesema kuwa  umasikini sio sifa, wala wao katika umoja wa UKAWA hawatamani umasikini, wakati wa kuamini viongozi masikini hapana. wanataka Tanzania iondoke katika umasikini kwa sababu umasikini ni laana.
“Nimalizie kusema kwa nini Lowassa, sisi tulifanya tafiti, kwa sababu taifa letu limeendeshwa kwa propaganda kwa muda mrefu, Lowassa kwa muda wa miaka 10 amekuwa muhanga wa propaganda za CCM.”Amesema Mbowe.
Naye Fredirick Sumaye amesema   ametoka chama cha mapinduzi, katibu mkuu alisema wao ambao hawatukuteuliwa hatukuwa na maadili, amesema  kama kipimo cha maadili ni mheshimiwa Kinana yeye atakuwa  mtakatifu.
Amesema  leo Lowassa ametoka CCM ameonekana hafai, lakini ni Kikwete  ndiye  aliyemfanya waziri mkuu wake, kuna Rais anaweka kiongozi ambae hafai? Lakini ni Lowassa huyuhuyu ndiye aliyemuingiza Kikwete Ikulu.
Kwa upande wake mgombea Urais wa UKAWA  Lowassa amesema  sera yake  itakuwa  Kipengele cha kwanza elimu, cha pili elimu na cha tatu elimu. Maneno haya ameyaazima kwa waziri mkuu wa Uingereza. Cha kwanza elimu itakuwa inagharamiwa na serikali kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo kikuu.
Eneo la pili la kilimo ili tuweze kutengeneza ajira za kutosha  na   eneo la   tatu  ni   kuweka  umuhimu afya iwe bora kwa akina mama na watoto wadogo.



Urais 2015: Zitto Kabwe azilipua CCM na UKAWA


Urais 2015: Zitto Kabwe azilipua CCM na UKAWA




Zitto Kabwe akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam.

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe leo amewalipua chama cha Mapinduzi CCM pamoja na  Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuwa  hawana jipya katika kinyanganyiro cha Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 25,2015.
Akizungumza na Waandishi wa Hababri leo  Zitto Kabwe amesema kwamba chama chake pekee ndicho kilichobeba ajenda ya kuwakomboa watanzania kutokana na  kuweka ajenda nne za msingi watakazozifanyika kazi endapo watafanikiwa kuchaguliwa kukliongoza taifa la Tanzania.
“Kama untaka siasa za Mbwembwe nenda CCM,Kama unataka siasa za ulaghai nenda UKAWA na kama unataka siasa za misingi siasa za issues ni ACT-Wazalendo” amesema Zitto Kabwe.
Amesema kwamba mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli katika kampeni zake anazungumzia hasa Barabara utadhani anakwenda kuwa Rais wa Barabara,  wakati   UKAWA wakiwa hawana jipya.
Chama chake kina ajenda nne ambazo
(i)Haki ya Watanzania kwenye hifadhi ya jamii kwa kupata bima afya,
(ii)Uchumi unaozalisha Ajira
(iii)Afya
(iv)Elimu

Wednesday, 26 August 2015

Serikali yapiga marufuku Mgombea urais kupanda daladala

Serikali yapiga marufuku Mgombea urais kupanda daladala


Mgombea Urais wa Ukawa Edward Lowassa akiwa amepanda dala dala jana jijini Dar es salaam.
Serikali kupitia jeshi la Polisi nchini Tanzania imepiga marufuku wagombea urais kupanda daladala ikiwa ni siku moja imepita tokea  mgombea urais wa Ukawa Edward Lowassa  na Mgombea Mwenza wake Juma Duni Haji kupanda daladala.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam  Kamanda wa Kanda maalumu jijini Dar es salaam Suleiman Kova amesema  jeshi la Polisi limepiga marufuku  wagombea urais kupanda dala dala kufuatia wananchi wengi  kuacha shughuli zao na kuelekea kwa wanasiasa hao suala linaloweza kuhatarisha usalama wao.
Katika  hatua nyingine Lowassa alipanda dala dala jana katika maeneo ya Gongo la Mboto kuelekea Chanika kujionea shida mbalimbali za wananchi hao akiwa na mgombea Mwenza wake Juma Duni Haji suala lililopelekea wananchi kufurahi kuwaona wagombea hao katika eneo hilo ambalo wamedai hakuna kiongozi aliyewahi kufika tangu nchi ipate uhuru mwaka 1961.

Waziri wa zamani Masha afikishwa Mahakamani

Waziri wa zamani Masha afikishwa Mahakamani

Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani Lawerence Masha(mwenye tisheti nyeusi) akishuka kwenye gari katika mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam leo.


Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani Lawrence Fortunatus Masha (katikati) akitolewa katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo, akishitakiwa kwa  kosa la kutumia lugha ya matusi na kejeli dhidi ya maafisa wa Polisi. 
Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani Lawrence Fortunatus Masha 47, leo  ameafikishwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, akishitakiwa kwa kutumia lugha ya matusi na kejeli dhidi ya maafisa wa Polisi.
Akisoma mashita dhidi ya mshitakiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Waliwandwe Lema, Mwendesha Mashitaka Wankyo Simon amesema mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Agosti 24 mwaka huu katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Upande wa Mashitaka umesema mshitakiwa alitumia lugha ya matusi na kejeli dhidi ya Inspekta Msaidizi Juma Mashaka na maafisa wengine wa polisi.
Kwa mujibu wa mashitaka, mshitakiwa alisema “Polisi ni washenzi waonevu hamna shukrani, huruma wala dini,” maneno ambayo yangeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Mshitakiwa amekana mashitaka hayo na upande wa mashitaka umesema uchunguzi bado unaendelea.
Mshitakiwa amepelekwa mahabusu kwa kile kilichodaiwa kusubiriwa kwa uthibitisho wa hati za wadhamini.
Miongoni mwa masharti yaliyotolewa na mahakama ili kupata dhamana ni kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika, watakaosaini dhamana ya shilingi milioni moja.
Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena Septemba 7 mwaka huu.

Tuesday, 25 August 2015

Lowassa awashitukiza soko la Tandika

Lowassa awashitukiza soko la Tandika


Mgombea urais wa Ukawa Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza Juma Duni Haji katika soko la Tandale.
Mgombea wa Urais wa Ukawa Edward Lowassa  pamoja na mgombea mwenza Juma Duni Haji leo wamewashitukiza wafanyabiashara  katika soko la Tandika jijini Dar es salaam.
Aidha, wagombea hao waliwasili katika soko hilo asubuhi ya leo ambapo shughuli zilisimama kwa muda, kabla ya kuanza mazungumzo na wafanyabishara  hao   alikaribishwa  chai  na mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo.
Ziara hiyo ya kushitukiza iliyoanzia Mbagala siku ya jana ni maalumu kwa lengo la kuzungumza na wananchi wa hali ya chini kuhusiana na matatizo yanayowakumba  katika maisha yao ya kila siku.

Nape aishukia ICC kuangazia uchaguzi mkuu Tanzania

Nape aishukia ICC kuangazia uchaguzi mkuu Tanzania


Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye.
Hivi karibuni  Muendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya kimataifa ya uhalifu  (ICC) Fatou Bensoudabbalisema kuwa wanaufuatilia kwa makini uchaguzi mkuu wa Tanzania ili  kuhakikisha hakuna haki za binadamu zitakazo kiukwa,
Akizungumzia kauli hiyo  Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema anadhani ni upuuzi kwa mahakama hiyo kusema inaangalia uchaguzi kwani si kazi yao.
Amesisitiza kuwa  kama kweli wanafuatilia mambo haya basi wafuatilie na nchi za ulaya. Hata hivyo zimeabaki siku  60 tu kufanyika kwa uchaguzi mkuu ambao unatarajia kufanyika oktoba 25.

Magufuli aikacha Helkopta, sasa ni mtaa kwa mtaa


Magufuli aikacha Helkopta, sasa ni mtaa kwa mtaa



Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli.
Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amesema katika  kampeni zake  atatumia barabara ili apate kuzifahamu kero za wananchi katika maeneo mengi ya nchi.
Licha ya kudai kuukacha usafiri huo amefafanua kuwa maeneo mengine yenye ulazima wa kutumia usafiri mbadala, anaweza kufanya hivyo
Akizungumza katika mkutano wake wa kwanza tangu kuzinduliwa kwa kampeni za chama hicho katika Kijiji cha Mishamo, kilichopo Kilometa 150 kutoka mkoani Katavi, Dk Magufuli alisema amekataa kutumia helikopta katika baadhi ya sehemu atakazofanya ziara, ili kujionea mwenyewe kero ya barabara inayowakabili Watanzania.
Akiwa katika   kijiji  cha  Mishamo, Magufuli pia aliwahakikishia wananchi wa maeneo hayo, ambao baadhi yao waliokuwa wakimbizi waliotoka Burundi wakati wa machafuko ya mauaji ya kimbari, lakini wakapewa uraia wa Tanzania, kwamba uongozi wake utaheshimu na utawatambua kuwa wao ni Watanzania.
Kwa upande wa sekta ya umeme  amesema waziri atakayemteua wa umeme, akishindwa kupeleka umeme Mpanda, atoke mwenyewe huku akisema atakuwa rais wa wanaChadema, wana ACT, wana CUF na wasio na chama kwa kuwa maendeleo hayana chama.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimezindua kampeni zake siku ya Jumapili ya Jumapili jijini Dar es salaam ambapo wagombea wake wametimkia mikoani kusaka kura za wananchi pamoja na kunadi sera zao.

Friday, 7 August 2015

Urais 2015:UKAWA yatikiswa, Dr. Slaa abeba siri nzito

Urais 2015:UKAWA yatikiswa, Dr. Slaa abeba siri nzito

Tarehe August 6, 2015
Dr.Wilbroad Slaa pamoja na Prof Ibrahim Lipumba.
Umoja  wa katiba  ya wananchi UKAWA umetikiswa leo kufuatia Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba kutangaza kujizulu kwa madai ya kushindwa kusimamia makubaliano yaliyopelekea kuundwa kwa umoja huo huku Naibu Katibu mkuu Chadema  Dr. Wilbroad  Slaa akiendelea  kuumiza  kichwa  umoja  huo.
Aidha, UKAWA iliyo onekana  kuimiza kichwa CCM usiku na mchana na sasa imeanza mpasuko mkubwa  baada ya Lipumba kuachia Ngazi huku Dr.Slaa akitangaza kuzungumzia hatma yake ukawa muda ukifika.
Uamuzi wa Prof. Lipumba kujiuzulu umepokelewa kwa masikitiko makubwa na wanachama wa CUF na Ukawa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.
Wakizungumza na Hivisasa Blog haya ndio baadhi ya maoni ya wanachama hao;
Jumanne Jumanne dereva Daladala kutoka maeneo ya Posta amesema kwamba amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za Prof. Lipumba kujiuzulu kwani alikuwa na matumaini makubwa na umoja huo lakini hivisasa ana baki kutazama tu mambo yanavyokwenda.
Anna Mwakibinga Mkazi wa Mnazi Mmoja amesema yeye kwa upande wake ni mwana chama wa CCM hivyo uamuzi huo Prof. Lipumba kung’atuka  anaona kama ni ukomavu wa demokrasia.
Jerome Haule mkazi wa Kariakoo  amesema kwamba hivisasa imani yake kwa vyama vya siasa imetoweka kwa kuwa  wanasiasa wa Tanzania hawaeleweki.
Mwajuma  Shabani  amesema kwamba ana tumaini vyama hivyo vitajipanga vizuri ili kuhakikisha kuwa  vina ondoa tofauti zao.
Katika hatua nyingine Maalim Seif ambaye ni Katibu mkuu wakati wa kutambaulishwa Edward Lowassa kama  Mgombea Urais alisema kwamba hajapata taarifa zozote za mwenyekiti huyo kujiuzulu lakini hata hivyo jana zilienea taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Prof.Lipumba ana mpango wa Kujiuzulu.
Kufuatia kukwama kwa mkutano wake  Prof. Lipumba na Waandishi wa Habari makao makuu ya CUF Buguruni jijini Dar es salaam mchana, ilipofika jioni Prof. Lipumba alijitokeza na kuzungumzia madai ya kuwa anataka kujiuzulu  kutokana na mamia ya wananchi kuzingira ofisi za CUF wakitaka kufahamau hatma ya kiongozi wao.
Licha Prof. Lipumba kukana madai lakini leo ametangaza rasmi kujiuzulu uenyekiti CUF  na kutangaza kuwa atajikita kufanya shughuli za kitaaluma kwa kujihusisha zaidi na ushauri wa masuala ya uchumi na maendeleo.
Kwa upande wa Dr Slaa, alipoulizwa kuhusu taarifa zilizozagaa kuwa maisha yake yapo hatarini kwa kuwa anatishwa, Dk Slaa alisema atalizungumzia muda ukifika.
Dk. Slaa aligombea urais mwaka 2010 na kushika nafasi ya pili baada ya Rais Jakaya Kikwete na ndiye aliyekuwa akitajwa kuwania tena nafasi hiyo kupitia Chadema na Ukawa kabla ya  kumteua Lowassa.
Kwa mujibu wa Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Bw.Tulizo Hendrick amesema kwamba migogoro inayoikumba UKAWA  ni dhahiri kuwa  ni neema kwa chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa wananchi wanapoteza imani na umoja huo.

Prof. Lipumba atangaza rasmi kujiuzulu Uenyekiti CUF

Prof. Lipumba atangaza rasmi kujiuzulu Uenyekiti CUF

Tarehe August 6, 2015
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba leo ametangaza rasmi kujiuzulu wadhfa huo na kusema kuwa atabaki kuwa mwanachama wa kawaida.
Profesa Lipumba amesema uamuzi wake unafuatia kushindwa kuafikiana na makubaliano yaliyofikiwa na vyama vinne shirikishi vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Amesema hafurahishwi na kufanya kile wanachokifanya wenzake kwa kuwa atakuwa anakwenda kinyume na makubaliano ya uongozi bora.
Vyama vinne vinavyounda umoja huo ni CUF, Chadema, NCCR Mageuzi na National League for Democracy (NLD).
Profesa Lipumba 63, amekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CUF kwa miongo miwili (1995 – 2015) na amegombea nafasi ya urais katika miaka ya 2000, 2005 na 2010.

KQ hoi: Inahitaji sindano ya trilioni 3 kupumua

KQ hoi: Inahitaji sindano ya trilioni 3 kupumua

Tarehe August 6, 2015
Kenya Airways (KQ), shirika la ndege la Kenya, na moja ya mashirika makubwa ya ndege barani Afrika iko hoi bin taabani.
Wiki iliyopita shirikahilo lilitangaza kupata hasara ya Shilingi za Tanzania bilioni 500, kiasi cha hasara kikubwa zaidi kwa kampuni kilichowahi kuripotiwa nchini humo.
Kufuatia taarifa hizo, sasa wataalam wa fedha wa Standard Investment Bank wametabiri kuwa kampuni ya KQ sasa inahitaji kiasi cha Shilingi Trilioni 2 za Tanzania kuweza kurudi katika hali ya kawaida ya uendeshaji.
Wiki iliyopita waziri wa Hazina wa Kenya Trotich alitangaza mpango wa serikali wa kuipa KQ Shilingi Trilioni 1 na bilioni 200 fedha ambazo zimepangwa kulisaidia shirika hilo kupunguza madeni yaliyoliemea kwa sasa.
Kutokana na hali mbaya ya shirika, inategemewa kuwa shirika hilo litalazimika kuchukuwa maamuzi magumu ya kujipanga upya, yakiwemo ya kupunguza wakubwa wake kwa kupunguza idadi ya ndege, wafanyakazi na hata safari.

Monday, 3 August 2015

Azam Bingwa Kagame Cup 2015

Azam Bingwa Kagame Cup 2015

Tarehe August 3, 2015
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidy Meckysadick (wa pili kushoto) akimkabidhi la ubingwa wa soka Afrika Mashariki na Kati, Kagame baada ya kuifunga Gor Mahia ya Kenya 2-0 leo uwanja wa Taifa jijini Dares salaam.
Timu ya azam imetangazwa bingwa wa michuano ya vilabu bingwa afrika mashariki CECAFA kagame cup baada ya kuifunga Gor mahia ya kenya katika fainali na kuondoka na kitita cha dola 30,000 pamoja na kikombe katika mchezo uliochezwa mapema leo jijini Dar es Salaam huku ikiweka rekodi ya kucheza michuano yote bila kufungwa ndani ya Dakika 90.
Azam iliingia fainali baada ya kuitandika KCCA ya Uganda goli 1-0 huku Gor Mahi ya kenya ikiingia fainali baada ya kuitandika Khartoum ya Sudan magoli 3-1 katika michezo ya nusu fainali.
Nahodha wa timu ya Azam John Bocco (Aderbayor )akipokea zawadi ya dola 30,000
John Bocco (Adebayor) alikuwa wa kwanza kuipatia Azam bao la kwanza akiunganisha krosi ya Kipre Cheche katika dakika ya 16 ya mchezo katika kipindi cha kwanza baada ya safu ya ulinzi ya Gor mahia inayoongozwa na Haruna Shakava kupotena na kumpa Bocco nafasi ya kufumania Nyavu.
Katika kipindi cha kwanza Bocco na Kipre walikosa magoli katika dakika tofauti huku kwa upande wa Gor Mahia Michae Olunga na Erick Ochieng wakipata wakati mgumu baada ya beki wa Azam Paschal Wawa kuonyesha kuwamudu wachezaji wote hao wa Gor Mahia na mpaka mapumziko Azam walikuwa mbele kwa Goli moja.
Wachezaji wakimbeba kocha wa Timu Stewart Halll mara baada ya Timu hiyo kutangwa mabingwa.
Katika kipindi cha pili Aucho Khalid wa Gor Mahia alionekana kuichezesha timu hiyo huku akitoa pasi nyingi za pembeni zilizokuwa zikimkuta Erick Ochieng lakini jitihada zake azikuzaa matunda na Aucho Khalid alimchezea madhambi Kipre Cheche katika eneo la hatari madhambi yalioyozaa goli katika dakika ya 64 ya mchezo katika kipindi cha pili.
Mpaka dakika ya 90 Azam waliibuka washindi wa Michuano hiyo wakiwachapa Gor Mahia ya Kenya Magoli 2-0 katika mchezo wa fainali.

Sunday, 2 August 2015

Mawaziri watano Waanguka kura za maoni CCM

Mawaziri watano Waanguka kura za maoni CCM

Tarehe August 3, 2015
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
Matokeo ya awali kura za maoni CCM yameonekana kuwa mwiba kwa mawaziri watano pamoja na baadhi wa wabunge kupitia chama hicho kufuatia kuangushwa  na kuchaguliwa wengine.
Mawaziri walio anguka ni  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Ambapo alipata kura  5,128 dhidi ya Hassan Masalla, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero aliyepata kura 6,444.
Aliyepata kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora na pia Waziri wa Katiba na Sheria akikwama katika mchakato wa kurejea bungeni, naibu wake katika Wizara wa Mambo ya Ndani, Pereira Silima naye ameanguka katika kura za maoni huko jimbo la Bumbwini, Unguja.
Mwanasiasa mwingine aliyekwama katika kura za maoni ni Mahadhi Juma Mahadhi ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  katika Jimbo la Paje, Unguja huku mshindi akiibuka kuwa Jaffar Sanya Jussa.
Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima naye  ameripotiwa kuanguka katika kura za maoni katija Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani.
Mwingine ni  Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Milton Makongoro Mahanga ambaye  baada ya kuanguka ametimkia Chadema.
Kutoka  Jimbo la Mvomero mkoani Morogoro, aliyewahi kuwa mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Suleiman Saddiq `Murad’ amefanikiwa kumwangusha mshindani wake wa siku nyingi, Amos Makalla ambaye alilitwaa jimbo hilo mwaka 2010.
Nalo Jimbo la Uzini ambako mwanasiasa nguli aliyepata kuwa waziri katika wizara mbalimbali za Serikali ya Muungano, Muhammed Seif Khatib ameshindwa katika kura za maoni.
Kwa upande wa  wabunge nao  wamekuwa na wakati mgumu majimboni kwao, akiwemo Ismail Aden Rage wa Tabora. Mbunge mwingine aliyeshindwa katika kura za maoni ni Mtutura Abdalla wa Tunduru Kusini.

clouds stream