Friday, 22 April 2016

Serikali: Rais Hawezi Kujipunguzia Mshahara

Serikali: Rais Hawezi Kujipunguzia Mshahara

Tarehe April 22, 2016Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Suala la mshahara wa Rais, limeibuka tena bungeni ambapo Bunge limeelezwa kwamba kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais hawezi kujipunguzia mshahara pindi anapoapishwa kushika wadhifa huo.
Akitoa taarifa kwa Bunge, Waziri Simbachawene alisema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake, Ibara ya 43, Ibara ndogo ya 3, Ukurasa wa 62 inamzuia Rais kupunguza mshahara akiwa madarakani.
Simbachawene alisema ibara hiyo inasema;  ‘Mshahara na malipo ya Rais, havitapunguzwa wakati Rais anapokuwa bado anashika madaraka yake. “Rais aliyepo sasa hawezi kujipunguzia mshahara wake yeye mwenyewe isipokuwa anapoondoka anaweza kuweka kiwango cha mshahara cha Rais ajaye.
Simbachawene alitoa maelezo yake akimjibu Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza (Chadema) aliyemuomba Rais John Magufuli kujipunguzia mshahara na kuanza kulipa kodi.
Akiwa nyumbani kwake Chato mkoani Geita wakati alipokwenda kwa mapumziko mafupi hivi karibuni, Rais Magufuli alijitangazia mbele ya umma kiwango cha mshahara anacholipwa akisema ni Sh milioni 9.5 kwa mwezi.

clouds stream