Kombora la Korea Kaskazini
Marekani, Japan na Korea ya Kusini wameomba kuwepo kwa mkutano wa dharura wa baraza la usalama la umoja wa mataifa ili kujadili jaribio la kombora la hivi karibuni lililofanywa na Korea ya Kaskazini katika bahari ya Japan.
Japan na Marekani zimelaani majaribio ya makombora ya masafa marefu yaliyofanywa na Korea Kaskazini katika bahari ya Japan.Rais Trump na kiongozi wa Japan, Shinzo Abe, walikuwa wanakutana mjini Florida pindi uzinduzi huo wa makomboro ulipofanyika.Bwana Abe amelielezea tukio hilo kuwa halivumiliki.
Kwa upande wake, Donald Trump amesema Marekani itashirikiana na Japan kwa asilimia mia moja.Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini nae, amesema jaribio hilo, ambalo linakiuka vikwazo vya umoja wa mataifa, linaonyesha azma ya Korea Kaskazini ya kukuza teknolojia ya makombora ya nuklia.
Raia huyu katika mji mkuu wa Korea Kaskazini wa Pyongyang, wanaonyesha jinsi wanavyounga mkono mpango wa kivita wa nchi yao, nchi yetu imeonyesha msimamo wake wazi, kwamba tutaendelea kujenga uwezo wetu wa kujilinda, kwa kutumia nguvu za nuklia, na uwezo wa kushambulia, katika kipindi ambacho maadui wetu wanaendelea na vikwazo vya kutugandamiza. Tutatetea amani na usalama wa nchi yetu kwa njia yoyote, kwa jitihada zetu wenyewe, na tutachangia amani ya dunia na utulivu."
Mshauri mwandamizi katika ikulu ya Marekani amesema serikali ya rais Trump ,itaimarisha ushirikiano muhimu katika eneo la pacific ili kuepusha hali ya uhasama kutoka Korea ya kaskazini.
Katika mahojiano ya televisheni, Stephen Miller amesema uhusiano mkubwa baina ya nchi mbili umeonyeshwa mwishoni mwa juma ambapo ziara ya waziri mkuu wa Japan kwa marekani, ambapo amekaa katika nyumba ya rais trump mjini Florida.