Saturday 25 February 2017

Simba Yaitafuna Yanga 2-1, Kichuya Awa mwiba kwa wana jangwani

C5g1cFAWgAU91WU
img-20161130-wa0008

Kwa mara ya tatu mfululizo timu ya Simba inamaliza mchezo dhidi ya Yanga katika Ligi Kuu Bara huku ikiwa pungufu katika ‘Dar Derby’ ambapo leo wana msimbazi hao wameikazia msuli Yanga na kuifunga goli 2 kwa ­1.

Simba sasa imefanikiwa kuondoka na pointi 4 katika michezo yao miwili dhidi ya watani zao Yanga baada ya kutoka sare katika mechi ya mzunguko wa kwanza na sasa inaongoza ligi hiyo kwa tofauti ya pointi 5.

Yanga ndio waliotawala mchezo wa leo kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha kwanza huku wakiisumbua safu ya ulinzi ya Simba mara kadhaa hali iliyopelekea mabeki wa Simba kujikuta wakifanya makosa madogomadogo yaliyowaletea balaa.

Ilikuwa dakika ya sita ambapo Yanga kupitia kwa mshambuliaji wake Simon Msuva ilipeleka kilio kwa wana msimbazi baada ya kuipatia timu yake goli  kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Simba Novalty Lufunga kumchezea madhambi Obrey Chirwa katika eneo la hatari.

Bao hilo lilidumu hadi mapumziko ambako katika kipindi cha pili Simba waliweza kucharuka na kutaka kusawazisha bao hilo kwa udi na uvumba.Wasanii, Mwana FA na Ommy Dimpoz wakifatilia mpambano huo.

Wasanii, Mwana FA na Ommy Dimpoz wakifatilia mpambano huo.

Vuta nikuvute hiyo ilishuhudia beki wa Simba, Jean Bukungu akilambwa kadi nyekundu dakika ya 54 na Muamuzi, Mathew Akrama kutoka Mwanza baada ya kumshika shati Obrey Chirwa akiwa mlinzi wa mwisho na kuisababishia Simba kubaki pungufu kwa mara ya tatu mfululizo dhidi ya watani zao Yanga.

Lakini kama ambavyo waswahili husema ‘Historia huwa inajirudia,’ kwa mara ya pili mfululizo Simba wameweza kutoka nyuma na kusawazisha bao dhidi ya Yanga huku wakiwa pungufu baada ya Laudit Mavugo kutikisa nyavu za Jangwani dakika ya 66 kwa mpira wa kichwa akimalizia krosi safi kutoka kwa Ajib.

Zaidi pia waswahili wanasema ‘Mtembea bure si sawa na mkaa bure,’ na usemi huo ulidhihirishwa na Chiza Kichuya dakika ya 81 pale alipopiga shuti kali kutoka nje kidogo ya eneo la hatari na mpira kukwamia katika nyavu za lango la Yanga na kuipatia Simba bao la pili.

Hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika Simba imeondoka na pointi 3 muhimu na kuwaacha watani zao Yanga wakimuwazia Kichuya na wasijue la kumfanya.16996292_1396063963790927_3820016781787035723_n

clouds stream