Monday, 6 February 2017

Trump ataka ukaguzi wa makini kufanywa mipakani

Maafisa wa ukaguzi katika uwanja wa ndege nchini Marekani

Maafisa wa ukaguzi katika uwanja wa ndege nchini Marekani
img-20161130-wa0008

Rais Donald Trump amewaagiza maafisa wa usalama wa mipakani kuwakagua kwa makini watu wanaoingia Marekani ,huku marufuku yake dhidi ya raia wa mataifa 7 ya kiislamu ikiwa imesimamishwa.

Mapema mahakama ya rufaa ilikataa ombi la serikali ya Marekani la kurejesha amri ya marufuku ya kuwazuia wahamiaji ambapo ofisi ya mwanasheria mkuu imepewa hadi leo Jumatatu kujibu maamuzi hayo.

Amesema kuwa mahakama ambayo imezuia hatua hiyo inafanya kuwa vigumu kuimarisha usalama katika mipaka ya Marekani na kumshtumu jaji aliyetoa uamuzi huo kwamba analiweka taifa hilo mashakani.

Amesema kuwa iwapo kutakuwa na tukio lolote jaji huyo na mfumo wote wa mahakama utalaumiwa.

clouds stream