Tuesday, 7 February 2017

Zitto Kabwe ‘Akesha’ Bungeni Kukwepa Polisi

Mbunge Zitto Kabwe.
Mbunge Zitto Kabwe.

img-20161130-wa0008Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT­Wazalendo Bw.Zitto Kabwe anadaiwa kukesha Bungeni kukwepa mkono wa dola kufuatia yeye kuwa mwanzilishi wa sakata la Baa la Njaa ambalo Serikali inasema ni uchochezi.

Kwa mujibu wa taarifa za awali zimebainisha kuwa Zitto ameamua kukesha ndani ya mjengo kuhofia kukamatwa na Askari wa Jeshi la Polisi ili afikishwe jijini Dar es salaam kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazomkabili.

Aidha Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alikamatwa mara baada ya kutoka nje ya Bunge na kuletwa jijini Dar es salaam ambapo anatarajiwa kusomewa mashitaka ya uchochezi leo katika mahakama ya Kisutu.

Baada ya Sakata la Njaa kuibuliwa Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt.Charles Tizeba Bungeni januari 31 alisema kwamba kuna halmshauri 55 zina uhaba wa chakula kufuatia tathmini iliyofanyika kutokana na ukosefu wa mvua katika baadhi ya maeneo hapa nchini.

clouds stream