Sunday, 5 February 2017

Chelsea yafunga ''kidomodomo'' cha Arsenal

Chamberlain wa Arsenal akizuiwa na wachezaji wa Chelsea

Chamberlain wa Arsenal akizuiwa na wachezaji wa Chelsea
img-20161130-wa0008

Chelsea imepanda pointi 12 juu ya kilele cha ligi ya Uingereza EPL baada ya kuinyamazisha Arsenal.

Marcos Alonso aliiweka kifua mbele Chelsea baada ya kufunga kwa kichwa kufuatia shambulio la Diego Costa.

The Blues baadaye waliongeza bao la pili dakika saba baada ya muda wa mapumziko baada ya Eden Hazard kuchenga safu ya ulinzi ya Arsenal na kufunga kwa urahisi.

Wenger atazama mechi hiyo akiwa katika eneo la mashabiki
Wenger atazama mechi hiyo akiwa katika eneo la mashabiki

Mchezaji wa zamani wa Chelsea Cesc Fabregas alimaliza udhia baada ya kipa Ceck kuifanya masikhara na kumpatia mpira wa bure.

Hatahivyo mshambuliaji wa Arsenal Oliver Giroud alifunga bao la kufutia machozi kwa niaba ya Arsenal katika dakika za mwisho za mechi.

clouds stream