Thursday, 16 February 2017

Ridhiwani Kikwete Atoa Ya Moyoni Sakata La ‘Unga’

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
img-20161130-wa0008

Sakata la Madawa ya kulevya lime endelea kuchukua mijadala hapa nchini ambapo Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete ametoa ya moyoni kuhusiana na Sakata hilo.

Akizungumza katika maohojiano na moja ya redio jijini hapa Ridhiwani amesema kuwa serikali inatakiwa kuiendeleza vita ya Madawa ya kulevya kama ilivyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda hadi ifike mwisho na kuyatokomeza kabisa hapa nchini.

Amesema Madawa ya kulevya yamepoteza maisha ya vijana wengi wenye uwezo mkubwa na mchango katika taifa ambapo amemtolea mfano msanii kama Langa aliyefariki dunia pamoja na shida anazozipata mwanamuziki Ray C.

Ridhiwani amesema yeyote atakayethibitika kuhusika, achukuliwe hatua, huku akionesha imani kubwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt Rogers William Sianga aliteuliwa hivi karibuni.

Kwa upande mwingine Ridhiwani amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kuanzisha vita hiyo na kutaka wahusika wachukuliwe hatua kali.

clouds stream