Thursday, 9 February 2017

Manji Atimiza Ahadi, Ajipeleka Central Kabla Ya Ijumaa Kufika

picha manji
img-20161130-wa0008

 Mfanyabiashara Yusuph Manji tayari amefika Kituo cha Polisi Kati kwa ajili ya mahojiano baada ya hapo jana kutajwa katika orodha ya watu 65 wanaojihusisha na biashara ama utumiaji wa madawa ya kulevya.

Orodha hiyo ilitajwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambapo mbali na Manji, vigogo wengine waliotajwa ni pampja na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Mchungaji wa Kanisa la Ufufufo na Uzima, Askofu Gwajima, Mbunge wa zamani wa Kinondoni, Idd Azan na wengine.

Akitaja majina hayo, Makonda aliwataka watuhumiwa hao kufika kituo cha polisi siku ya kesho Ijumaa lakini Manji akasema kama ana uhakika na analosema kwanini asubiri hadi Ijumaa na kuahidi kuripoti kituoni hapo siku inayofuatia ya Alhamisi ambayo ni leo.

Manji anadaiwa kuwasili kituoni hapo na mawakili 6, wanne wakiwa wa kigeni na wawili wazawa

clouds stream