Sunday, 12 February 2017

JPM Awaapisha Makamishna Dawa Za Kulevya, Uhamiaji Na Mabalozi

16508005_1383276638402993_544378440421370196_n
img-20161130-wa0008

Rais, Dkt. John Pombe Magufuli  amemuapisha Rogers William Sianga kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na Kuzuia Madawa ya Kulevya na wasaidizi wake wawili.

Pia amewaapisha Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Jenerali Dkt. Anna Makalala na mabalozi watatu.

 Mabalozi hao ni Omary Yususph Mzee (Algeria), Joseph Sokoine (Ubelgiji) na Grace Mgovani (Uganda). 

Amemtaka Kamishna Mkuu wa kupambana na dawa za kulevya kufanya kazi bila kuogopa ili kuweza kuokoa nguvu kazi ya taifa inayoteketea.

Rais Magufuli akimuapisha Rodgers William Sianga kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Rais Magufuli akimuapisha Rodgers William Sianga kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya.

Ameongeza kuwa vita dhid ya dawa hizo ni ngumu kwa sababu ina faida kubwa na hivyo wafanyabiashara wa dawa hizo wanaweza kufanya chocote kwa fedha zao na kuongeza kuwa kama isingekuwa sheria imesema yeye mwenyewe angekua mwenyekiti wa timu ya kupambana na dawa hizo.

‘They can do anything at any cost,’ lazima tushirikiane katika vita hii,” amesema Rais Magufuli.

Amemtaka Waziri wa Mambo ya Nje na mabalozi katika nchi ambazo kuna watanzania wamekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na madawa ya kulevya wasijihusishe katika kuwatetea wahalifu hao kwa namna yoyote ile na kuacha sheria zifuate mkondo wake.

Aidha, amewataka waandishi wa habari na wanamitandao kuweka Utanzania mbele na pale anapotokea mtu anapambana na dawa za kulevya wamuunge mkono badala ya kumchafua.

“Vita hii ya dawa ya kulevya ni kubwa sana na hatuwezi kwenda nayo kimzahamzaha na Serikali itahakikisha inasimamia vyema Sheria ya Mwaka 2015 ya Madawa ya Kulevya,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amemtaka Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna kufanya mabadiliko makubwa ndani ya Idara ya Uhamiaji kutokana na utendaji kutoridhisha.

“Nataka ufanye mabadiliko makubwa Uhamiaji izalishe fedha, ukadhibiti utoaji ‘Passport’ maana zimekuwa zikitolewa kiholela,” amesema Rais Magufuli.

clouds stream