Thursday, 9 February 2017

Gwajima Afunguka Sakata La Madawa Ya Kulevya

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima.
img-20161130-wa0008

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima ametoa ya Moyoni kufuatia jina lake kutajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuwa anahusika na masuala ya Madawa ya Kulevya.

Akizungumzia sakata hilo Gwajima amesema kwamba hilo ni shambulio kwa kanisa la Ufufuo na Uzima sio kwa Gwajima.

“Makonda alikuja kanisani kwangu na marehemu Samwel sitta na akapanda mazabauni je hakujua kama nauza unga?”Amehoji Gwajima.

Amesema alikuwa mkali sana kwa serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Dkt.Jakaya Kikwete hivyo basi haamini kabisa kwamba Rais Dkt.John Pombe Magufuli amemtuma Makonda kumdhalilisha.mbele ya umma ili aonekane hafai.

“Wenzetu wabunge wameungana kutumia sheria na kanuni zao watamuhoji sisi raia wa kawaida tusio na sheria wala kanuni za kututetea tutashtaki wapi? .”Amehoji Gwajima.

Ameongeza kuwa hili ni shambulio kwa wote walio okoka, Maaskofu wote, Wachungaji wote ili waonekane kuwa hawafai katika jamii.

Amesisitiza kuwa Makonda atavuka mipaka, atakemea Polisi, atakemea Jeshi, atakemea Wabunge na hadi Waziri Mkuu.

Gwajima amemuomba Rais Dkt Magufuli ambadilishie kazi Makonda kwa madai kuwa hii ya Ukuu wa Mkoa kutawala na kuongoza hata watu asiowapenda imemshinda.

Askofu Gwajima ana waumini zaidi ya elfu sabini kanisani kwake akiwa na Makanisa zaidi ya 400 nchi nzima ikiwemo jiji la Dar es salaam.

clouds stream