Monday, 8 December 2014

MESSI APIGA ‘HAT TRICK’ BARCELONA IKIUA MTU 5-1,KOCHA LIVERPOOL: HATUWEZI KUMTEGEMEA GERARD ,MTIBWA SUGAR WAPELEKA MSIBA MSIMBAZI, WAIGONGA SIMBA 4-2


MESSI APIGA ‘HAT TRICK’ BARCELONA IKIUA MTU 5-1




Mshambuliaji Raia wa Argentina, Lionel Messi, Jana ameongoza safu ya ushambuliaji kunako klabu yake ya Barcelona na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 5-1 dhidi ya Espanyol, Huku nyota huyo aking’ara kwa kutupia bao 3, Hat Trick.
Katika mchezo huo ambao ulipigwa ndani ya Uwanja wa Camp Nou, Espanyol ndio walianza kupata goli kupitia kwa Sergio Garcia dakika ya 13 kabla ya Messi kusawazisha bao hilo dakika ya 45 na kufanya timu hizo zienda kupumzika zikiwa sare ya 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo kwa mara ya pili Messi akawarudisha kati wenzake kwa kufunga bao la 2 dakika ya 50, zilipita dakika 3 tu, Pique akaiandikia Barcelona bao la tatu kunako dakika ya 53.
Pedro naye hakuwa nyuma katika mchezo huo kwani kunako dakika ya 77 aliiandikia timu yake bao 4 kabla ya Lionel Messi kumaliza kazi kwa kupachika bao la 5 kwa timu yake huku kwake likiwa ni bao la 3 dakika 81.

KOCHA LIVERPOOL: HATUWEZI KUMTEGEMEA GERARD




Kocha mkuu wa klabu ya Liverpool Brenda Rodgers amewaonya wachezaji wake kwa kusema kuwa hawatakiwi kumtegemea nahodha wa timu hiyo Steven Gerrard kila mechi.
Rodgers amesema kuwa wachezaji hao wanafaa kuziba pengo la nahodha huyo bila wasiwasi wakati ambapo hayupo katika timu.
Gerrard mwenye umri wa miaka 34 alipumzishwa kwa mara ya pili mfululizo katika mechi ya nyumbani iliyokamilika bila kwa bila.
Licha ya kiungo huyo wa kati kuchezeshwa kunako dakika ya 67 hakuweza kubadilisha mambo uwanjani Anfield.
”Hatuwezi kila mara kumtegemea, haiwezekani kwamba kila mechi yeye ndiye atakayesababisha mchezo mzuri ama mabao”,alisema Rodgers.

MTIBWA SUGAR WAPELEKA MSIBA MSIMBAZI, WAIGONGA SIMBA 4-2




Klabu ya Simba leo imeambulia kipigo cha bao 4-2 kutoka kwa vinara wa ligi kuu ya Tanzania bara Mtibwa Sugar kutoka Manungu, Tuliani, Morogoro katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es salaam.
Katika mchezo huo Simba ndio walianza kupata bao kupitia kwa Said Demla kipindi cha kwanza lakini halikuchukua muda mrefu Mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi akaisawazishia Mtibwa katika dakika ya 28.
Katika kipindi cha pili Mtibwa waliongeza kupeleka msiba Msimbazi baada ya Mohammed Ibrahim kuiandikia timu yake bao la pili dakika ya 51 na dakika ya 53, kabla ya Ame Ally kufunga la nne dakika ya 78.
Dakika ya 89 mshambuliaji Amisi Tambwe alifunga bao la pili kwa Simba kwa mkwaju wa penati nakufanya matokeo yawe 4-2.
Mchezo huo kwa Simba ilikuwa ni kipimo katika kuelekea mchezo wa Nani mtani jembe hapo Desemba 13 wiki kesho, huku wakiwa wametoka kutoa sare ya 0-0 na Express ya Uganda juzi kunako uwanja wa Taifa.

KESI YA SHEIKH PONDA KUSIKILIZWA LEO,RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO YA WAKUU WA MIKOA TANZANIA,ZITTO KUIBUA KASHFA KUBWA ZAIDI YA ESCROW 2015

KESI YA SHEIKH PONDA KUSIKILIZWA LEO


Kesi ya Sheikh Ponda inasikilizwa asubuhi hii mkoani Morogor. Sheikh Ponda anakabiliwa na kesi ya  uchochezi   iliyotokea  Mkoani Morogoro.
Hatua hiyo inafuatia mara baada  ya  kuachiwa  huru kutokana na  kesi  ya madai ya Ardhi ya Agrekanza inayomilikiwa na Afidhi Self  iliyokuwa inamkabili jijini Dar es salaam. Katika kesi hiyo  Mahakama ilijiridhisha   kuwa  Sheikh Ponda hakuwa na  hatia.

RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO YA WAKUU WA MIKOA TANZANIA



Wakuu wa mikoa takribani 6 nchini Tanzania wamehamishwa vituo vya kazi huku mkuu wa mkoa 1 mmoja mpya akiongezeka katika safu ya wakuu wa mikoa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na  Katibu mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kwamba  Rais Kikwete amemteua mkuu wa Wilaya ya Karatu mkoani  Arusha Bw. Daudi Felix Ntibenda kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha.
Wakuu wamikoa wengine waliohamisha vituo vya kazi ni Bw. Elaston  Mbwilo  kutoka mkoa wa  Manyara  kwenda mkoa wa Simiyu. Bw. Mbilo anachukua nafasi ya Paschal Mabiti aliyepewa likizo kutokana na ugonjwa. Bw.Joel Nkanga Bendera amehamishiwa mkoani Manyara akitokea mkoa wa Mororgoro. Dkt Rajabu M. Rutengwe anayehamishiwa mkoa wa Morogoro kutoka mkoani Tanga.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa wengine ni Bw. Magagula  Saidi  Magagula kutoka mkoa wa Lindi kwenda mkoa wa Tanga. Mwantumu  Bakari  Mahiza anakwenda  mkoani  Lindi akitokea mkoani Pwani pamoja na Mhandisi Evarist B. Ndikilo  anakwenda  mkoani Pwani kutoka mkoa wa Arusha.
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa mpya Bw Ntibenda ataapiwa leo Ikulu jijini Dares salaam ambapo wakuu wa mikoa wengine watabakia katika vituo vyao vya kazi.

ZITTO KUIBUA KASHFA KUBWA ZAIDI YA ESCROW 2015



Sakata lingine litakalohusu kashfa nne kubwa zaidi ya ESCROW  kuibuka  mwakani kufuatia kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC)  kukamilisha ufisadi uliofanyika katika akaunti ya Escrow. Katika sakata hilo Bunge limetaka serikali kuwawajibisha  Mawaziri pamoja na watendaji wa serikali na kuendeleza uchunguzi kwa waliopata mgao wa fedha ambazo ni zaidi ya bilioni 306.
Kwa mujibu wa Mwenyikiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Zitto Kabwe amesema kwamba  kamati  yake  itatumia  mwezi desemba na januari mwakani  kupitia ripoti nne ambazo zina maslahi kwa Taifa.
Akinzungumzia kashfa hizo, Zitto amesema kuwa kashifa hizo ni za utoaji vibali vya kuagiza sukari na kuingiza  sukari  nchini,  ripoti  nyingine  ni uchunguzi wa ubinafsishaji wa Benki ya NBC, ripoti maalumu ya Bandari  pamoja  na  mikataba ya gesi.
Sakata la utoaji wa Vibali vya sukari,  imebainika kuwa  ufisadi wake ni mkubwa kuliko hata sakata la ESCROW lilionekana kuteka hisia za watanzania kwa takribani wiki moja. Hatua hiyo inatokana na baadhi ya wamiliki wa viwanda vya sukari nchini Tanzania  kutangaza kuwa wana mpango  wa kuvifunga viwanda  vya sukari kutokana na kuviendesha kwa hasara kwa kuwa kuna ushindani mkubwa wa  soko la sukari  kutokana na kuruhusu wafanyabiashara kuingiza kutoka nje ya nchi.

Monday, 1 December 2014

Je, Unahisi Mungu Yuko Karibu na Wewe?

MNARA WA MLINZI DESEMBA 2014

 

HABARI KUU | UNAWEZA KUMKARIBIA MUNGU

Je, Unahisi Mungu Yuko Karibu na Wewe?


“Kuwa na uhusiano mzuri na Mungu kunakufanya uhisi usalama, utulivu, na amani. Unahisi kwamba Mungu anakutakia mema siku zote.”—CHRISTOPHER, MWANAMUME KIJANA NCHINI GHANA.
“Mungu hukuona unapoteseka, naye anakupenda kuliko unavyoweza kuwazia.” —HANNAH, MSICHANA MWENYE UMRI WA MIAKA 13, ALASKA, MAREKANI.
“Inafariji na kufurahisha sana kutambua kwamba una uhusiano mzuri na Mungu!”—GINA, MWANAMKE KUTOKA JAMAIKA MWENYE UMRI WA MIAKA 40 HIVI.
Watu wengi huhisi kama Christopher, Hannah, na Gina. Wanaamini kwamba Mungu ni rafiki yao. Vipi wewe? Je, unahisi kwamba uko karibu na Mungu? Au, je, unataka kumkaribia au kuboresha uhusiano wako na Mungu? Huenda ukajiuliza hivi: ‘Inawezekanaje mwanadamu awe na uhusiano mzuri na Mungu Mweza-Yote? Ikiwa inawezekana, jinsi gani?’

INAWEZEKANA KUMKARIBIA MUNGU

Biblia inasema kwamba inawezekana kuwa na uhusiano mzuri na Mungu. Pia inasema kwamba Mungu alimwita Abrahamu, aliyekuwa Mwebrania ‘rafiki yake.’ (Isaya 41:8) Pia kumbuka mwaliko unaotolewa kwenye andiko la Yakobo 4:8: “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi.” Kwa hiyo, ni wazi kwamba inawezekana kuwa na uhusiano mzuri au urafiki na Mungu. Lakini kwa sababu hatuwezi kumwona Mungu, inawezekanaje ‘kumkaribia’ na kuwa na uhusiano mzuri pamoja naye?
Ili kupata jibu la swali hilo, fikiria jinsi urafiki kati ya wanadamu unavyositawishwa. Kwa kawaida, watu hujuana majina na kisha kuanzisha urafiki. Halafu, kadiri wanavyoendelea kuwasiliana ndivyo urafiki wao unavyositawi. Urafiki wao huzidi kuimarika wanapoendelea kutendeana mambo mema. Ndivyo ilivyo pia tunapotaka kuwa na uhusiano mzuri na Mungu. Acheni tuchunguze jinsi ya kufanya hivyo.

clouds stream