KESI YA SHEIKH PONDA KUSIKILIZWA LEO
Kesi ya Sheikh Ponda inasikilizwa asubuhi hii mkoani Morogor. Sheikh Ponda anakabiliwa na kesi ya uchochezi iliyotokea Mkoani Morogoro.
Hatua hiyo inafuatia mara baada ya kuachiwa huru kutokana na kesi ya madai ya Ardhi ya Agrekanza inayomilikiwa na Afidhi Self iliyokuwa inamkabili jijini Dar es salaam. Katika kesi hiyo Mahakama ilijiridhisha kuwa Sheikh Ponda hakuwa na hatia.
RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO YA WAKUU WA MIKOA TANZANIA
Wakuu wa mikoa takribani 6 nchini Tanzania wamehamishwa vituo vya kazi huku mkuu wa mkoa 1 mmoja mpya akiongezeka katika safu ya wakuu wa mikoa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kwamba Rais Kikwete amemteua mkuu wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha Bw. Daudi Felix Ntibenda kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha.
Wakuu wamikoa wengine waliohamisha vituo vya kazi ni Bw. Elaston Mbwilo kutoka mkoa wa Manyara kwenda mkoa wa Simiyu. Bw. Mbilo anachukua nafasi ya Paschal Mabiti aliyepewa likizo kutokana na ugonjwa. Bw.Joel Nkanga Bendera amehamishiwa mkoani Manyara akitokea mkoa wa Mororgoro. Dkt Rajabu M. Rutengwe anayehamishiwa mkoa wa Morogoro kutoka mkoani Tanga.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa wengine ni Bw. Magagula Saidi Magagula kutoka mkoa wa Lindi kwenda mkoa wa Tanga. Mwantumu Bakari Mahiza anakwenda mkoani Lindi akitokea mkoani Pwani pamoja na Mhandisi Evarist B. Ndikilo anakwenda mkoani Pwani kutoka mkoa wa Arusha.
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa mpya Bw Ntibenda ataapiwa leo Ikulu jijini Dares salaam ambapo wakuu wa mikoa wengine watabakia katika vituo vyao vya kazi.
ZITTO KUIBUA KASHFA KUBWA ZAIDI YA ESCROW 2015
Sakata lingine litakalohusu kashfa nne kubwa zaidi ya ESCROW kuibuka mwakani kufuatia kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) kukamilisha ufisadi uliofanyika katika akaunti ya Escrow. Katika sakata hilo Bunge limetaka serikali kuwawajibisha Mawaziri pamoja na watendaji wa serikali na kuendeleza uchunguzi kwa waliopata mgao wa fedha ambazo ni zaidi ya bilioni 306.
Kwa mujibu wa Mwenyikiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Zitto Kabwe amesema kwamba kamati yake itatumia mwezi desemba na januari mwakani kupitia ripoti nne ambazo zina maslahi kwa Taifa.
Akinzungumzia kashfa hizo, Zitto amesema kuwa kashifa hizo ni za utoaji vibali vya kuagiza sukari na kuingiza sukari nchini, ripoti nyingine ni uchunguzi wa ubinafsishaji wa Benki ya NBC, ripoti maalumu ya Bandari pamoja na mikataba ya gesi.
Sakata la utoaji wa Vibali vya sukari, imebainika kuwa ufisadi wake ni mkubwa kuliko hata sakata la ESCROW lilionekana kuteka hisia za watanzania kwa takribani wiki moja. Hatua hiyo inatokana na baadhi ya wamiliki wa viwanda vya sukari nchini Tanzania kutangaza kuwa wana mpango wa kuvifunga viwanda vya sukari kutokana na kuviendesha kwa hasara kwa kuwa kuna ushindani mkubwa wa soko la sukari kutokana na kuruhusu wafanyabiashara kuingiza kutoka nje ya nchi.