MESSI APIGA ‘HAT TRICK’ BARCELONA IKIUA MTU 5-1
Mshambuliaji Raia wa Argentina, Lionel Messi, Jana ameongoza safu ya ushambuliaji kunako klabu yake ya Barcelona na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 5-1 dhidi ya Espanyol, Huku nyota huyo aking’ara kwa kutupia bao 3, Hat Trick.
Katika mchezo huo ambao ulipigwa ndani ya Uwanja wa Camp Nou, Espanyol ndio walianza kupata goli kupitia kwa Sergio Garcia dakika ya 13 kabla ya Messi kusawazisha bao hilo dakika ya 45 na kufanya timu hizo zienda kupumzika zikiwa sare ya 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo kwa mara ya pili Messi akawarudisha kati wenzake kwa kufunga bao la 2 dakika ya 50, zilipita dakika 3 tu, Pique akaiandikia Barcelona bao la tatu kunako dakika ya 53.
Pedro naye hakuwa nyuma katika mchezo huo kwani kunako dakika ya 77 aliiandikia timu yake bao 4 kabla ya Lionel Messi kumaliza kazi kwa kupachika bao la 5 kwa timu yake huku kwake likiwa ni bao la 3 dakika 81.
KOCHA LIVERPOOL: HATUWEZI KUMTEGEMEA GERARD
Kocha mkuu wa klabu ya Liverpool Brenda Rodgers amewaonya wachezaji wake kwa kusema kuwa hawatakiwi kumtegemea nahodha wa timu hiyo Steven Gerrard kila mechi.
Rodgers amesema kuwa wachezaji hao wanafaa kuziba pengo la nahodha huyo bila wasiwasi wakati ambapo hayupo katika timu.
Gerrard mwenye umri wa miaka 34 alipumzishwa kwa mara ya pili mfululizo katika mechi ya nyumbani iliyokamilika bila kwa bila.
Licha ya kiungo huyo wa kati kuchezeshwa kunako dakika ya 67 hakuweza kubadilisha mambo uwanjani Anfield.
”Hatuwezi kila mara kumtegemea, haiwezekani kwamba kila mechi yeye ndiye atakayesababisha mchezo mzuri ama mabao”,alisema Rodgers.
MTIBWA SUGAR WAPELEKA MSIBA MSIMBAZI, WAIGONGA SIMBA 4-2
Klabu ya Simba leo imeambulia kipigo cha bao 4-2 kutoka kwa vinara wa ligi kuu ya Tanzania bara Mtibwa Sugar kutoka Manungu, Tuliani, Morogoro katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es salaam.
Katika mchezo huo Simba ndio walianza kupata bao kupitia kwa Said Demla kipindi cha kwanza lakini halikuchukua muda mrefu Mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi akaisawazishia Mtibwa katika dakika ya 28.
Katika kipindi cha pili Mtibwa waliongeza kupeleka msiba Msimbazi baada ya Mohammed Ibrahim kuiandikia timu yake bao la pili dakika ya 51 na dakika ya 53, kabla ya Ame Ally kufunga la nne dakika ya 78.
Dakika ya 89 mshambuliaji Amisi Tambwe alifunga bao la pili kwa Simba kwa mkwaju wa penati nakufanya matokeo yawe 4-2.
Mchezo huo kwa Simba ilikuwa ni kipimo katika kuelekea mchezo wa Nani mtani jembe hapo Desemba 13 wiki kesho, huku wakiwa wametoka kutoa sare ya 0-0 na Express ya Uganda juzi kunako uwanja wa Taifa.