Lowassa: ’ Hakuna wa kukata jina langu CCM’
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa amesema kuwa hatarajii jina lake kukatwa
katika vikao vya Chama cha Mapinduzi(CCM) vitakavyoketi julai kumteua mwanasiasa atakaye peperusha bendeara ya chama hicho katika kinyang’anyiro cha urais mwezi oktoba mwaka 2015.
Akizungumza mara baada ya kuwasili mkoani Ruvuma Lowassa amesema anaamini Chama chao kitatenda haki kwa kurudisha jina lake kuwa mgombea urais wa Tanzania.
“Nimekuwa mwanaCCM tangu mwaka 1977 nilipomaliza chuo kikuu, sijawahi kufanya kazi nje ya CCM hivyo nakijua chama na hakuna mgombea atakayeweza kuvunja rekodi ya utendaji wangu katika chama, sasa leo anayetaka kukata jina langu anatoka wapi? anakata kwa sababu gani? Sioni kosa la kukatwa jina na Watanzania hawaoni, kwa hiyo msiwe na wasiwasi jina litarudi tu”. alisema Lowassa.
Akiwa mkoani Ruvuma Lowassa amepata wadhamini ambao ni wanaCCM zaidi ya elfu 52.