Urais 2015: Membe awatisha watangaza nia CCM

Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la
Mtama, Bernard Membe pamoja na mke wake wakiusalimia umati wa wana CCM
na wakazi wa Lindi, katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana
Akizungumza na mamia ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya CCM Mkoa wa Lindi jana Membe ametamba kuipeleka nchi katika uchumi wa viwanda unaobebwa na kilimo na kuahidi kujenga serikali ya waadilifu.
Amesema kabla ya kuchukua uamuzi wa kufikiria urais alijipima na kuona anatosha kwa nafasi hiyo, pia baada ya kuwaangalia wagombea wenzake wote anaamini yeye ndiye mwenye sifa za kustahili kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Tanzania.
Amesisitiza kuwa uadilifu wake ni wa kuzaliwa, uwajibikaji usio wa kawaida na ndiyo sababu kila uchaguzi wananchi wa Jimbo lake la Mtama wamekuwa wakimchagua kwa idadi kubwa ya kura.
Kwa upande wa uzoefu amesema ana uzoefu mkubwa baada ya kuwa Ofisa usalama wa Taifa kuanzia mwaka 1978, Ofisa Ubalozi,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Naibu Waziri wa Nishati, Waziri wa Mambo ya Nje kuanzia Desemba mwaka 2006 hadi sasa.