Monday, 15 June 2015

Mafuriko Georgia, hofu yatanda wanyama wakali waranda mitaani

Mafuriko Georgia, hofu yatanda wanyama wakali waranda mitaani

Tarehe June 15, 2015
518884300-Zoo-Animals-Escape-in-Georgia-Floods
Mafuriko katika mji mkuu wa Georgia yameua watu 12 huku hatari zaidi ikiwa ni wanyama wakali kama Simba, nyani chui  na mbwa mwitu kutoroka kwenye zoo walikokuwa wameifadhiwa na kuingia mtaani huku polisi wakiwaomba wananchi kukaa ndani huku wakifanya jitiahada za kuwawinda wanyama hao.
Hofu ilizidi kutanda kwenye mji huo wenye idadi ya watu milioni 1.1 baada ya mafuriko hao kuacha idadi kubwa ya watu wakiwa hawana makazi na wanyama wakali kama mbwa mwitu na wengine wakili wakiwa bado hawajakatwa hivyo kuzua hofu kubwa ya kudhuru binadamu kutokana kuwa na njaa.
Tukio hili licha ya kukutwa miili ya wafanyakazi 3 wa zoo hiyo ila mkurugenzi wa Zoo amesema anasikitika sana kuona moja ya kivutio kikubwa kwenye zoo hiyo simba mdogo mweupe kwa jina la Shumba kupigwa risasi.
Maafisa bado wanajitaidi kuwasaka wanyama hao waliotoroka kwa kutumia helikopta wanaamini watarudisha mji huo kwenye hali ya amani kwa wakazi wake.

clouds stream