Migiro ajitosa kuchukua fomu ya Urais leo
Tarehe June 15, 2015
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Asha-Rose Migiro leo anatarajia kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) majira ya saa tisa mchana akifuatiwa na kada mwingine wa chama hicho Salum Marupu.
Aidha, Migiro, atakuwa mwanamke wa nne kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo ya juu ya kuiongoza nchi kwa miaka mitano ijayo wakiwemo Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Marekani, Amina Salum Ally.
Mwingine ni aliyekuwa Mbunge wa Iringa na pia alishakuwa Naibu Waziri wa Fedha, Monica Mbega, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dk Mwele Malecela.