Wakristo,Waislamu wahimizwa upendo
Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya pili Mzee Ally Hassan Mwinyi amewataka waislam hapa nchini kuepuka shari,chuki na uadui baina yao na waumini wengine wasio kuwa waislam na badala yake wapende kuwa na amani,utulivu na mshikamano ambao umetufikisha hapa kuanzia nchi yetu ilipopata uhuru mwaka 1961.
Aidha, Mzee Mwinyi amesema hayo kwenye ghafla ya ufunguzi wa msikiti mpya wa masjid Suhaib Ruumi uliojengwa kilimani Hewa Wilayani Nachingwea kwa msaada wa Taasisi ya Al-Hikima Education Centre ya jijini Dar es salaam.
Akizungumza mara baada ya ufunguzi Mwinyi amesema kuwa msikiti ni sehemu ya ibada na kupata mafundisho ya mwenyezi mungu na siyo vinginevyo hivyo aislamu waache falaka badala yake wakae pamoja na kufanya ibada kwa pamoja kwa ajili ya mwenyezi mungu na pia kulinda amani na utulivu tulionao.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ngazi ya mkoa wa lindi na wilaya ya Nachingwea akiwemo waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mathias Chikawe ambae nae alitoa shukrani kwa niaba ya wananchi na waislam wa Nachingwea.