Tuesday, 10 November 2015

HESLB yawatangazia neema wanafunzi vyuo vikuu

HESLB yawatangazia neema wanafunzi vyuo vikuu

Tarehe November 10, 2015
Moja ya chuo kikuu nchini Tanzania.
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza kutoa mikopo kwa waombaji wenye sifa wapya 40,836 kati ya waombaji 50,830  mwaka wa masomo wa 2015/2016 walio omba mikopo hiyo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, George Nyatega amesema  hadi sasa imekwishawapangia mikopo jumla ya waombaji mikopo wenye sifa 40,836 wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2015/2016.
“Majina ya waombaji waliofanikiwa kupata mikopo kutoka katika awamu zote mbili yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa olas.heslb. go.tz na tovuti ya Bodi (www.heslb. go.tz),” alisema Nyatega
Katika awamu ya kwanza, HESLB ilitoa orodha yenye jumla ya waombaji 12,282 waliopata mikopo hiyo ikifuatiwa na waombaji wengine wapya 40,836.
Bodi hiyo imewasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu wakati mchakato wa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa unaendelea.
Ameongeza kuwa  orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili  huku lengo la Bodi hiyo likiwa  ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wenye sifa ya kupata mikopo katika mwaka wa masomo 2015/2016 ambao ni 50,830, wote wanapata mikopo.
Katika hatua nyingine Nyatega aliwataka Watanzania kupuuza taarifa zisizo za kweli zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba, HESLB, haitatoa mikopo kwa waombaji wapya.

clouds stream