Tuesday, 10 November 2015

Rais Kagame ‘aishutumu’ Burundi kisa mauaji ya Raia

Rais Kagame ‘aishutumu’ Burundi kisa mauaji ya Raia

Tarehe November 9, 2015
Rais wa Rwanda Paul Kagame pamoja na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Rais wa Rwanda Paul Kagame ameshutumu vikali viongozi wa Burundi kutokana na mauaji yanayoendelea nchini humo na kuonya kuwa huenda kukatokea mauaji ya halaiki
Kagame ameshangaa ni vipi viongozi wa taifa hilo jirani “wanaweza kuruhusu wananchi wao kuuawa kiholela.
Rais Kagame alisema hayo Ijumaa, lakini hotuba  yake haikutangazwa hadi mwishoni mwa wiki  wakati  akihutubia katika hafla ya kuwatunuku Wanyarwanda waliosaidia kuwaficha na kuwaokoa Watutsi wakati wa mauaji ya kimbari 1994 pamoja na wanaharakati wanaotetea umoja na maridhiano miongoni mwa Wanyarwanda.
Akizungumza kwa Kinyarwanda Rais Kagame alisema: ”Tazama nchi jirani kama Burundi, maisha yao yamesimama kabisa. Lakini sababu ni ipi? Wana historia inayofanana na yetu. Ila viongozi wao wapo kwa ajili ya kuua wananchi kuanzia asubuhi hadi jioni.”
Rais akijifungia sehemu isiyojulikana, hakuna anayejua sehemu alikojificha, hakuna anayezungumza naye, huyo anaongoza watu vipi?” alisema Bw Kagame,
”Watu wanakufa kila siku, maiti zinazagaa  barabarani  kinachosikitisha ni kuwa bara la Afrika lina ugonjwa wake lenyewe kiasi kwamba hata nitalaumiwa eti nimekosea kuitaja nchi nyingine, eti ningechezea diplomasia au siasa. Siyo haki mimi nitasema wazi”Alisema Kagame
Amesisitiza  kuwa Viongozi wanashinda wakiua watu, maiti zinatapakaa sehemu zote; wakimbizi wanarandaranda sehemu  watoto, wanawake kisha wanasema ni siasa. Hiyo ni siasa gani?”Amehoji Kagame.
Uhusiano kati ya Rwanda na Burundi umekuwa wa kusua sua  sana tangu Bw Nkurunziza atangaze kuwa atawania urais kwa muhula wa tatu, hatua iliyopingwa na wapinzani. Katika hatua nyingine Mwezi uliopita, Burundi ilimuondoa  Balozi mmoja kutoka Rwanda ikimtuhumu kwa kuhujumu usalama wa nchi hiyo.

clouds stream