Magufuli aanza kwa kuwashitukiza Wizara ya Fedha
Rais Dkt.Magufuli akisaini kitabu cha wageni Wizara ya Fedha jijini Dares salaam leo.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli leo ameanza kazi kwa kuwashitukiza watendaji wa wizara ya fedha.Aidha, Magufuli ametembea kwa miguu kutoka Ikulu jijini Dar es salaam
hadi wizara ya Fedha akiwa ameongozana na maofisa wa usalama ambapo mara
baada ya kufika katika ofisi ya Wizara ya Fedha aliwakuta maofisa
wengine wakiwa nje ya ofisi zao.Inadaiwa huenda akatembelea wizara nyingine za serikali yake kujionea utendaji kazi wa wafanya kazi katika serikali yake mpya ya awamu ya tano.