Friday 6 November 2015

Mikutano ya CCM, Chadema yapigwa marufuku nchini

Mikutano ya CCM, Chadema yapigwa marufuku nchini

Tarehe November 7, 2015
Wafuasi wa CCM na UKAWA, pande mbili kubwa zinanzochuana katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba 25.
Wafuasi wa CCM na UKAWA, pande mbili kubwa zilizochuana katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba 25.
Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano na mikutano ya vyama vya siasa iliyokuwa imepangwa kufanyika kwa nyakati tofauti kwa madai ya kuwepo na hali tete ya  kisiasa.
Kwa mujibu wa  msemaji wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Advera Bulimba amesema, polisi imefikia hatua hiyo kutokana na hali ya kisiasa ilivyo kwa sasa.
Amesema  vyama vya CCM na Chadema tayari vilikuwa vimeshawasilisha maombi ya kufanya mikutano na maandamano sehemu mbalimbali hapa nchini.
SSP Bulimba ameongeza  kuwa,  kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na vyombo vya usalama nchini  hali ya kisiasa kwa sasa nchini bado si nzuri kwani bado kuna mihemko mikubwa ya kisiasa kufuatia uchaguzi mkuu uliomalizika wiki iliyopita.
“Baadhi ya Vyama vya Siasa vimekuwa vikiomba kufanya mikutano ya hadhara na maandamano nchi nzima kwa siku moja na vingine maandamano yasiyo na kikomo. Katika hali ya kawaida hili halikubaliki,”amesema SSP Bulimba na kuongeza:
Amesisitiza kuwa tathmini iliyofanywa na vyombo vya usalama imebaini kuwa bado kuna mihemko mikubwa ya kisiasa  hivyo kufanyika mikutano hiyo kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Jeshi la Polisi nchini bado linasisitiza katazo lake la awali la mikutano na maandamano hadi hapo hali ya kisiasa itakapotengamaa.”Amesema Bulimba
Kwa upande mwingine Jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani na kuwasihi kuendelea na shughuli zao za maendeleo.

clouds stream